Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabdhi Luninga kwa Wajasiliamali wa BBC katika Mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama |
Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi fedha kwa ajili
ya kebo ya TV muda mfupi baada ya kukabidhi Luninga kwa kijiwe cha Kahawa cha BBC katika Mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa
Shinyanga Khamis Mgeja jana amekabidhi msaada wa luninga yenye thamani ya
shilingi 260,000/= kwenye kijiwe maarufu cha wajasiliamali cha Kahawa
maarufu kwa jina la BBC kilichopo katika mji mdogo wa Isaka Wilayani Kahama wakati
akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
Wajasiriamali hao walimwomba mwenyekiti
huyo wa CCM msaada huo wa Luninga ili waweze kupata habari kupitia chombo hicho
hasa nyakati za asubuhi na jioni kabla ya kazi na baada ya kazi ili kwenda
sambamba na mambo yanatokea ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na wajasiriamali hao baada ya
kukabidhi luninga hiyo Mgeja aliwataka wazee na vijana kujenga utamaduni wa
kuridhika na vipato vidogo wanavyovipata kulingana na hali waliyonayo badala ya
kukimbilia vipato vya juu ambavyo vipo nje ya uwezo wao wa kimahitaji.
Kufuatia msaada huo mwenyekiti wa
Wajasilimali hao wa BBC Ally Salumu Msangi alishukuru na kuongeza kuwa msaada
huo umefika katika kipindi muafaka hasa wakati wa kipindi hiki cha bunge la
katiba linaloendelea mjini Dodoma.
|
Social Plugin