MJAMZITO wa miezi saba Bi. Mwanaidi Athumani mkazi wa Chamwino
Morogoro hivi karibuni alifanya mchepuko wa kutoka nje ya ndoa na
kujikuta akijifungua mtoto wa kiume ndani ya gesti iliyopo maeneo ya
Mafisa mjini Morogoro.
Habari zinasema kuwa mwanamke huyo alifanya mchepuko huo baada ya
mumewe kusafiri kwenda kutafuta fedha za maandalizi ya kujifungua kwake.
Bila ya kujali kama ana mimba ya miezi saba, Mwanaidi aliingia katika
gesti moja (jina tunalo) akiwa na mwanaume anayedaiwa kufanya kazi ya
kupiga debe katika stendi ya Msamvu na mambo yalipomwendea kombo,
mwanaume huyo akatimua mbio.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Mwanaidi na mpiga debe wake walipanga
katika chumba namba 3 na baada ya kufanya mambo yao, Mwanaidi akaanza
kupiga kelele kutokana na kushikwa na uchungu. Ilimbidi mhudumu wa gesti
hiyo, Bi. Moshi Eliya afike kumsaidia Mwanaidi aweze kujifungua salama
pamoja na kwamba hakuwa na ‘gloves’ wala kitu chochote cha kulinda afya
yake.
Chanzo chetu ambacho nacho kilikuwa ni mpangaji ndani ya gesti hiyo
kilisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8 usiku na Mwanaidi alipiga
kelele huku akizozana na mpiga debe wake. Kiliposikia tukio hilo, chanzo
hicho kikapiga simu kwa paparazi wetu aliyetinga katika nyumba hiyo ya
wageni kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.
Baada ya kujifungua salama, paparazi wetu alimuuliza Mwanaidi
kilichotokea ndipo mwanamke huyo akafunguka kuwa alikuwa amechepuka nje
ya ndoa baada ya kukumbwa na shetani.
“Nina mume na tuna watoto watatu huyu ni wanne, mume wangu amesafari
kwa ajili ya kutafuta fedha za maandalizi ya ujuo wa mwanetu akijua nina
mimba ya miezi saba,” alisema mwanaidi.
Pamoja na kutaka kugoma, lakini
mwandishi wetu alimchukua mwanamke huyo na kichanga chake na kuwapeleka
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako wamelazwa kwa uchunguzi zaidi.
Mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya ambaye alikuwa mkunga wa
Mwanaidi alisema kuwa alishindwa kutumia ‘gloves’ wakati wa kumzalisha
mzazi huyo kwa kuwa alikumkuta mtoto ameshaanza kutoka. “Mtoto
aliashaanza kutoka, hata hivyo kwa usiku ule tungepata wapi hizo
gloves?” alihoji.
Na Dustan Shekidele, Morogoro