Moja kati ya matukio makubwa yaliyoteka ‘attention’ ya watu wengi ni picha na video zilizowekwa kwenye ukurasa wa Facebook na boss wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma zikimuonesha mwimbaji toka Mwanza PNC akiwa amepiga magoti na kuonesha ishara ya mikono kama anaomba mbele ya boss huyo aliyetulia kwenye kochi akiwa amekunja 4.
Picha
na video hizo ziliwekwa na Ostaz Juma mwenyewe kwenye ukurasa wake wa
Facebook na kuandika, ““hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba
msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati.”
Haikuchukua
muda, watu mbalimbali ambao ni wadau wa muziki wa kizazi kipya walipaza
sauti wakilaani kitendo hicho kupitia mitandao ya kijamii wakiwemo
wasanii mbalimbali ambao hawakusita kumchana Ostaz kwa kile
kilichoonekana kuwa ni kumdhalilisha mwimbaji huyo.
Lakini
wapo mashabiki ambao waliporomosha matusi kufuatia tukio hilo na habari
hiyo kusambaa kwa nguvu kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyompelekea
Ostaz kudai kuwa siye aliyeziweka picha hizo. Lakini kilichowashitua
wengi baadae, ni pale ilipoonekana post nyingine kwenye ukurasa wake
akiwaponda watangazaji wa Tanzania na wasanii kuwa wanasumbuliwa na
njaa.
“Naona
watu mmeguswa sana na mimi kuanika picha ya PNC katika mitandao et,
tatizo wasanii wa Tanzania mnanjaa sana kuanzia watangazaji Radio na
wasanii njaa ndizo zinazo wasumbua...”
Lakini
baadae aliongea na Moko Biashara aka One B wa Times Fm kueleza kuwa
ukurasa wake metekwa na wezi wa akaunti za watu mtandaoni (hackers) na
kwamba hiyo sio post yake.
“Daah,
nshachanganyikiwa rafiki yangu watu wamehack akaunti yangu wanaandika
matusi wanatukana watu..hadi hapa mimi nimeshachanganyikiwa hadi hata
kuongea siwezi bro.” Alisema Ostaz.
Nadhubutu
kusema kwa msisitizo kuwa picha hizo ziliwekwa na Ostaz Juma kwa jinsi
nilivyozifanyia utafiti na kuzingatia kauli yake aloyoniambia kwa mara
ya kwanza, “Ndio PNC kunipigia magoti na kuniomba radhi, lakini sasa
mimi nikaamua kuwaonesha watanzania kwamba PNC amerudi kweli kuniomba
msamaha. Je, kama kweli PNC alikuwa analalamika ‘Ostaz anafanya kazi
zake hanijali hanisaidii…”
Hata
hivyo sina uhakika…huenda kweli hakuandika kauli ya kuwaponda
watangazaji na wasanii…nasema huenda kwa kuwa muda mchache baada ya
kudai kuwa akaunti yake ilikuwa imetekwa na hackers na kubadili
‘password’, aliingia tena na kuifuta post hiyo na kuandika nyingine ya
kuomba radhi na kueleza kuwa ilikuwa imetekwa kwa kipindi kile. Kwa
upande wangu ‘no comment’ kwenye hilo.
Anyways, kwa maelezo yote hapo juu bila shaka umepata picha nzima ya tukio hilo japo kwa ufupi.
Sasa
niende moja kwa moja kwenye mada na lengo langu, mkasa huu unapaswa
kuwa zaidi ya somo la kawada kwa Ostaz Juma na wengine hasa watu maarufu
ambao huichukulia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram
n.k kama sehemu fulani tu ya kuandika unachotaka kama jinsi ulivyopewa
uhuru ‘What’s on your mind’. Kumbe unatakiwa kufikiria sana kabla
hujaandika na sio kuandika tu kile kilichoko kichwani kwako, kama
unajali.
Ntatumia fikra ambazo nadhani alikuwa nazo Ostaz Juma kabla hajayaona matokeo ya alichokifanyana, matokeo yaliyomchanganya.
Huenda
Ostaz Juma alikuwa bado anafikiria kuwa Radio, Television na magazeti
pekee ndio vyombo vya habari vikubwa kuliko ‘social media’, wazo ambalo
ni la kizamani kwa dunia ya sasa hivi.
Huenda
Ostaz alikuwa hafahamu kuwa hivi sasa kwa kiasi kikubwa Traditional
Media kama Radio, Television na magazeti zimeungana na ‘New Media’
ambazo ni mitandao ya kijamii, tovuti pamoja na blogs na habari husambaa
kwa nguvu kupitia vyombo hivyo huku vikibadilishana.
Habari nyingi zina-break kwenye mitandao bila kujali muda na huzua mijadala mikubwa kama hiyo.
Huenda
alikuwa hafahamu kama, unachoandika Facebook kikishachukuliwa na watu
wakaanza kushare hata ukifuta bado kitaendelea na kufika mbali zaidi na
hata watu kuhamishia kwenye magroup ambayo huwa na maelfu ya watu au
hata kuhamishiwa ‘watsapp’ na huenda wakati unajitetea watu hao
wasisikie ama wakakupuuzia.
Huenda
yeye aliona ana marafiki 2,258 akaona sio watu wengi na kwamba
isingekuwa issue serious kiivo kama ambavyo angesema kwenye radio na
vituo vya television.
Huenda
alikuwa hafahamu kama picha inaongea lugha zote duniani (universal
language) hata bila kufuatilia nani kaandika nini. Hata mchina atakuwa
ameielewa picha hiyo kwa lugha yake!
Ngoja nimfungue macho kama kweli alikuwa anafikra hizo.
Hadi
kufikia mwishoni mwaka jana, takwimu zilionesha kuwa watu zaidi ya
billioni 1.2 duniani kote wanatumia Facebook na kwamba hao ni active
members, na kwa wastani kila mtumiaji ana marafiki zaidi ya 130 ambao
anaweza ku-share nao habari na ikasambaa duniani kote kwa muda mfupi.
Takwimu
hizo zinaonesha kuwa takribani asilimia 60 ya watu wazima wanaingia
kwenye mitandao mbalimbali ambapo hata kama hawajajiunga na mitandao ya
kijamii wanatembelea tovuti mbalimbali ambazo zinachukua habari kwenye
mitandao ya kijamii.
Habari
kama hizo zinazotokea Facebook huendelea kusambaa pia kwenye mitandao
mingine ya kijamii kama Instagram, na hata Twitter ambayo inachukua 18%
ya watumiaji wote wa mitandao, ambao wengi wao ni ‘active users’ na ndio
kundi kubwa la watu wenye ushawishi (influential) kama watu maarufu.
Twitter ina watumiaji zaidi ya milioni 640.
Kwa
upande wa Instagram, kwa mfano Diamond akiishare picha hiyo wataiona
watu zaidi ya 90,000 ambao wanaweza pia kushare, na huenda watu
wakaiamini moja kwa moja habari hiyo kuwa kuwa msanii wanaempenda
kalaani kitendo hicho.
Kwa
takwimu hizo, ni vyema kufahamu kuwa kupitia mitandao ya kijamii
hususani watu ambao wanafanya biashara inayotokana na kuuza kazi
zilizobebwa na ‘image’ yao kama vile kazi za muziki, wanaweza
kutengeneza biashara kubwa kwa kuwa wateja wengi wanaoweza kufanya
maamuzi wako kule.
Uamuzi
wa kuandika kitu kwenye mitandao ya kijamii kwa watu wenye biashara
kama hiyo nikitolea mfano wa Ostaz Juma lazima uwe unamnyima uhuru wa
kuandika kila anachofikiria tu, bali kuwaza mara mbili ama tatu matokeo
ya kuweka mtandaoni kile anachofikiria.
Mtu
kama Ostaz ambaye anawasaidia wasanii wa Tanzania, anatakiwa kufahamu
kuwa msaada wake kwa wanamuziki hao kwao ni biashara ambayo inahitaji
zaidi ya pesa kwa kuwa wanauza vitu viwili ambavyo ni muziki na ‘image’.
Uropokaji wa mambo unaweza kuvunja image ambayo kuijenga itamgharimu
msanii huyo zaidi ya pesa alizopewa kurekodi wimbo, kushuti video,
kupigishwa pamba na hata pesa ya promotion.
Kwa mtu maarufu anayetegemea kuuza kutokana na sapoti ya watu, anatakiwa kufahamu kuwa ukurasa wake wa Facebook sio kijiwe cha washikaji zake ambacho anaweza kusema chochote kilicho kichwani kwake bila kujali na wakakipotezea baadae.
Ingawa
Radio, Television na magazeti inawafikia watu wengi zaidi duniani na
ina nguvu, ni vyema kwa mtu kama Ostaz na wengine wenye nafasi katika
jamii kuelewa kuwa kila chombo cha habari kina nguvu kubwa na sio vyema
kukilinganisha na chombo kingine ama kukipuuza.
Yale yalitokea sebuleni kwake (Ostaz Juma) yalipaswa kuwa faragha kwao wote wawili na sio kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Mwisho,
ni vyema kwa mtu yeyote kutumia kanuni ya mitandao ya kijamii kuwa
usiandike kitu chochote kwenye mtandao wa kijamii ukiwa na hasira ama
ukiwa ‘too emotional’. Jitahidi kuvumilia kukaa nacho moyoni kwa muda na
baada ya kutafakari unaweza kushare na watu.
Social Plugin