Hafidhi kabla na baada ya kutumia Metakelfin
Hafidh Masokola mwenye umri wa miaka 47, mkazi wa Tabora amedai
kuwa alitumia dawa aina ya Metakelfin miaka minne iliyopita kwa lengo la
kutibu ugonjwa wa malaria, lakini dawa hizo zilimsababishia madhara
makubwa katika ngozi yake na kumpelekea kuwa albino.
Hafidh ambaye ni mjasiriamali
ameeleza kuwa alinunua dawa hizo ‘Pharmacy’ na kwamba baada ya
kumsababishia madhara hayo ameamua kujiunga na chama cha maalbino
Tanzania kwa kuwa anafanana na albino wengine.
Ameeleza kuwa katika hatua za awali za dalili mbaya ya ngozi yake,
alimuona daktari wa ngozi wa mkoa wa Tabora na alipewa ushauri ambao
hata hivyo baada ya kuufanyika kazi hali iliendelea kuwa mbaya.
“Ikabidi nikamuone daktari wa ngozi wa mkoa wa Tabora, anaitwa Dr.
George. Nikaenda nikamuonesha zile dalili, akaniambia hii itakuwa tube
za hydrocotzone baadae itapotea hiyo, basi mimi nikatumia zile tube za
hydrocotzone, lakini ikawa hainisaidii kitu. Matokeo yake yale
malengelenge yakaamia kwenye mguu, juu ya unyayo lakini yalikuwa hayana
dalili zozote za muwasho….” Ameeleza.
“Nikaanza utaratibu wa kupakaa mafuta ya Vaseline muda kama wa wiki
mbili hivi, lakini kikawa naona kama nikipakaa kwenye viganja…lakini
hayaoneshi kama mafuta unapakaa, yanazama moja kwa moja kwenye ngozi.
Ukipakaa kama dakika moja hivi ukipakaa unaona kama hujapakaa…” Hafidhi ameeleza.
Msikilize hapa kufahamu mkasa mzima ulivyokuwa,akiongea na Times fm