Mtangazaji
wa Channel Ten, Salum Mkambala (pichani) amepata ajali ya gari ambalo alikuwa
akiendesha kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro.
Kwa mujibu
wa mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten amesema kuwa Mkambala alipata
ajali hiyo maeneo ya Chalinze alfajiri ya leo na hali yake inaelezwa kuwa ni
mahututi baada ya kuumia vibaya. Haijafahamika yuko hospitali gani kwani
alikuwa peke yake kwenye gari na taarifa ilitolewa na msamaria mwema kwa simu
ya Salum na baada ya hapo simu yake haipatikani tena.....
Chanzo-GPL
Social Plugin