Aliyekuwa
tabibu msaidizi wa Dispensari ya Tumaini mjini Singida, (wa mbele)
Godlisten Raymond (37) na mfanyabiashara wa mbuzi na biashara ya kusaga
nafaka (wa tatu mbele) Adamu Shaban Hole (46) mkazi wa kijiji cha
Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,wakisindikizwa na askari
polisi kwenda gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kila mmoja kifungo cha
miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtoa mimba mwanafunzi na
kusababisha kifo chake.
MAHAKAMA
Kuu kanda ya kati iliyomaliza vikao vyake hivi karibuni mjini
Singida,imewahukumu aliyekuwa tabibu msaidizi wa dispensari ya Tumaini
Godlisten Raymond (37) adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya
kupatikana na hatia ya kujaribu kutoa mimba kwa njia isiyo sahihi kwa
mwanafunzi na kusababisha kifo chake.
Mshitakiwa
Godlisten anadaiwa kumtoa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi
Kintandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi, Hamida Athumani (16)
septemba saba mwaka 2006 na alifariki dunia septemba 17 mwaka huo huo
wa 2006, siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya
msingi.
Pia
katika kesi hiyo,mfanyabiashara wa mbuzi na kusaga nafaka mkazi wa
kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,Adamu Shabani Hole
(46),naye amepewa adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya
kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi Hamida Athumani (16) na
kisha kushiriki kutoa mimba hiyo na kusababishia kifo mwanafunzi huyo.
Ilidaiwa
mahakamanai hapo kuwa mshitakiwa wa pili ambaye ni mfanyabiashara ya
mbuzi,Adamu,katika kipindi hicho hicho,aliweza kumpa mwanafunzi mwingine
Rukia Juma aliyekuwa akisoma darasa moja na Hamida (marehemu).
Rukia
baada ya kutolewa mimba na washitakiwa,aliweza kulazwa katika
hospitali ya mkoa mjini hapa,na aliweza kunusurika kufariki dunia baada
ya kupatiwa matibabu.
Kabla
ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwendesha mashitaka wakili wa serikali
mkuu mfawidhi kanda ya Singida,Neema Mwanda,aliiomba mahakama hiyo itoe
adhabu kali ya kifungo cha maisha jela kwa washitakiwa,ili iwe
fundisho kwao na watu wengine wanaotarajia kuwatoa mimba wasichana
wadogo na kisha kusababisha vifo vyao.
“Vitendo
vya watu wazima kufanya mapenzi na wanafunzi na kisha kuwapa
ujauzito,havikubaliki kabisa,kwa sababu zinaharibu maisha ya wanafunzi
husika na wakati mwingine vinasababisha vifo.Pia madaktari na tabibu
wasaidizi wenye tabia ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama,nao
wanakwenda kinyume na sheria za taaluma zao”,amesema Mwanda.
Kwa
upande wake wakili wa kijitegemea kutoka Dodoma mjini.Deus Nyabiri
aliyekuwa anamtetea mshitakiwa wa kwanza,Godlisten,aliiomba mahakama
hiyo impe adhabu nafuu mteja wake ikizingatia kuwa kosa hilo ni la
kwanza kwake na pia anategemewa na familia yake na ya wazazi wake ambao
kwa sasa,wana umri mkubwa.
Naye
wakili wa kujitegemea wa mjini hapa,Raymond Kimu aliyekuwa akimtetea
mshitakiwa wa pili,Adamu,aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja
wake na kiwezekana imwachie huru,kwa madai kuwa baada ya kuwapa mimba
wanafunzi wawili waliokuwa darasa la saba,mke wake amemkimbia na familia
yake imemtega.
Akitoa
adhabu hiyo,jaji Cresentia Makuru, amesema kwa mazingira ya
kawaida,kosa walililofanya washitakiwa, hawastahili huruma ya mahakama.
Amesema
vitendo vya wasichana wadogo kupoteza maisha kwa kutolewa mimba kwa
njia isiyo salama,licha ya kusababisha vifo vyao,pia vinachangia ndoto
za wazazi kwa watoto wao,kupotea.
Aidha,jaji
Makuru amesema katiba ya nchi,inatamka wazi kwamba uhai wa mtu ni
lazima uheshimiwe na kulindwa.Hata sheria za kimataifa nazo zimetamka
hivyo hivyo.
Na Nathaniel Limu, Singida