Utafiti
uliofanywa na wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Sussex, Uingereza
umebaini kuwa Ndovu ni moja kati ya wanyama wenye kumbukumbu hasa katika
kutambua na kutofautisha sauti za binadamu kati ya mwanamke na
mwanaume.
Katika
utafiti huo ambao ulifanyika katika mbuga ya wanyama ya Amboseli nchini
Kenya, imegundulika kuwa ndovu wana uwezo mkubwa pia wa kutambua sauti
za watu wa makabila mbalimbali.
Ndovu
wamejifunza kutambua sauti za watu kutokana na kuwepo mzozo wa maji
kati ya binadamu wanaoishi karibu na mbuga hiyo na wanyama hao. Hivyo
ndovu wameweza kugundua sauti za binadamu wa makabila ambayo ni adui na
tishio kwao na wale ambao sio adui kwao.
Maasai
wa eneo la Amboseli wanaelezwa kuwa huwa na tabia ya ukali na huwaua
ndovu hao tofauti na Wakamba ambao wanakisiwa kuwa watulivu.
Zoezi
lilifanyika hivi, wakati ndovu hao wanaposikia sauti ya Maasai walirudi
nyuma na kujikusanaya kama wamesikia ishara ya hatari laikini
waliposikia sauti za Wakamba walibaki mahala pale pale kwa utulivu.
Hivyo
matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa ndovu wameongeza uwezo mkubwa wa
kurudisha kumbukumbu ili kutambua tofatuti kati ya sauti kadhaa za
makabila mbali mbali duniani.