|
Ni katika eneo la ofisi ya afisa mtendaji kijiji cha Kagongwa kata ya Kagongwa katika moja vituo vya kuchotea maji muda mchache tu baada ya kukata utepe kuzindua mradi wa maji katika vijiji vya Kagongwa na Iponya.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja na wakazi wa eneo hilo wakishuhudia tukio zima la uzinduzi rasmi wa mradi huo wakati wa kilele
cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa
|
|
Mkuu wa mkoa
akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wajumbe wa kamati ya maji katika kijiji cha Kagongwa
bi Annastazia Mayai muda mchache tu
baada ya kuzindua rasmi mradi huo wa maji.
|
|
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akimtwisha ndoo ya maji
bi Regina Nyanda kwenye eneo la mradi wa maji katika kijiji cha Kagongwa ikiwa
ni kiashirio cha kwamba sasa wananchi 11,294 wa vijiji vya Kagongwa na Iponya
wanaanza kunufaika na mradi huo na kuwapunguzia adha ya muda mrefu ya maji.
|
Awali kabla
ya mkutano wa hadhara,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiweka
jiwe la msingi katika tenki la mradi wa maji ambayo chanzo chake ni kisima
kirefu katika kijiji cha Kagongwa na Iponya katika kata ya Kagongwa wilaya ya
Kahama Mkoani Shinyanga.Mradi huo wa maji umeanza kujengwa tarehe 11,Juni 2013
na utarajiwa kukamilika Machi 30 mwaka huu,ikiwa jumla ya gharama za mradi huo
ni shilingi 432,884,055/= na pindi ukikamilika watu 11,294 watanufaika na mradi
huo.Kulia ni Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja.
|
Msanii wa
nyimbo za asili maarufu kwa jina la MWANAKWELA kutoka Kahama akiwa na kikundi
chake wakitoa burudani katika eneo la mkutano wa hadhara ulifanyika katika
ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Kagongwa na kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa
wa Shinyanga,wakuuwa wilaya zote za Shinyanga,wajumbe wa kamati za ulinzi na
usalama,wenyeviti wa halmashauri,wakurugenzi wa mamlaka za serikali za
mitaa,wakurugenzi watendaji wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira
mkoa,viongozi wa dini na siasa,wanahabari,wananchi n.k
|
|
|
|
Eneo la mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kagongwa wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kinajiri |
|
Jukwaa kuu wakiangalia burudani iliyokuwa inaendelea katika sherehe za siku ya maji duniani. | |
|
|
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza leo wakati kilele cha
maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema
ujenzi wa miradi ya maji mkoa Shinyanga ni kilelezo cha utekelezaji wa ilani
chama cha mapinduzi huku akiwapongeza viongozi mkoani Shinyanga kuanzia ngazi
ya chini kabisa hadi mkoa kwa kufanikisha miradi ya maji,kati ya miradi hiyo
vyake ni maji kutoka ziwa victoria,visima virefu na vifupi na visima vya
asili.Mgeja pia alimwaga sifa kwa serikali ya awamu ya nne chini ya rais Jakaya
Kikwete kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile
maji,barabara,hospitali,zahanati n.k.
|
|
Injinia wa
maji mkoa wa Shinyanga bi Elizabeth Kingu akiwasalimia wakazi wa wilaya ya
Kahama wakati kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa,ambapo mambo kadha
wa kadha yamesisitizwa na viongozi ni wananchi kutunza miundo mbinu ikiwa ni
pamoja kupanda miti katika maeneo ya miradi ili kutunza uoto wa asili lakini
pia kulipia ankara zao za maji kwa wakati na kuwa tayari kuchagia miradi hiyo
ya maendeleo ili iwe endelevu
|
|
Wanachi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye pamoja mambo mengine alisema maudhui ya ya kauli mbiu ya wiki ya maji mwaka huu ya UHAKIKA WA MAJI NA NISHATI yanatokana na ukweli kwamba maji na nishati vinategemeana kwani inaonesha kuwa asilimia kubwa ya nishati huzalishwa kwa nguvu ya maji na pia karibu asilimia 8 ya nishati duniani hutumika kuendesha mitambo ya kuazlisha maji,kutibu maji na kusukumia maji hadi yanapohitajika |
|
Mkuu wa mkoa
wa Shinyanga Mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga akitoa hotuba yake leo wakati wa
kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa yaliyofanyika wilayani
Kahama,ambapo alisema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kwa kiasi kikubwa
kuwahamasisha wananchi kuhusu utekelezaji wa sheria,sera na programu za maji
zinazoendelea hapa nchini.Alisema katika utekelezaji wa sera ya maji ya mwaka
2002 umelenga kuboresha usambazaji wa huduma za maji ,utunzaji wa mazingira na vyanzo
vya maji na uchangiaji wa gharama za miradi ya maji pamoja na gharama za
uendeshaji na matengenezo.
|
Mkuu wa mkoa
wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga alitumia fursa hiyo kuipongeza halmashauri ya
wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kutekeleza vizuri miradi ya maji kimkoa
na nchi nzima kupitia mpango wa BRN ambapo wananchi wanatakiwa kuchangia
asilimia 2.5 ya gharama za miradi ya maendeleo hususani fedha za kuanzia
shughuli za uendeshaji pindi miradi inapokamilika.Amesema Kishapu imefanya vizuri kwa kuchangia shilingi 56,840,000/= kati ya
sh.97,503,149/= sawa na 58%, na halmashauri mwisho katika ya 6 za mkoani Shinyanga
ni ile ya manispaa ya Shinyanga ambayo
imechangia shilingi 3,534,000/= kati ya sh.55,677,900/= sawa na 6.3%.
|
| |
|
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika kuboresha huduma ya maji mijini,mkoa wa Shinyanga unaendelea kushirikiana na mamlaka tano za maji safi na usafi wa mazingira ambazo ni KASHWASA,SHUWASA,KUWASA,Isaka na Mhunze.
|
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga Justine Sheka akizungumza
kwa niaba ya wenyeviti wa halmashauri 6 za wilaya mkoani Shinyanga ambapo
aliipongeza viongozi wa CCM kushirikiana na viongozi wa mkoa hadi ngazi za
chini katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezwa katika jamii
|
|
|
Mkuu wa mkoa
wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho ya wiki ya maji duniani akikabidhi pesa zilizotokana na mchango
watu mbalimbali waliofika katika sherehe hizo kwa ajili ya kuvipa nguvu vikundi
vya burudani vilivyokuwa katika sherehe hizo,jumla ya shilingi laki 1 na elfu 47
zilipatikana ,kila kikundi kikapewa kiasi chake,wengine elfu 30,wengine elfu
25.Pichani ni MWANAKWELA akipokea pesa kutoka kwa mkuu wa mkoa,Lakini hapo
anashikana mkono na mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja baada ya kuchukua pesa
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553