Mahakama ya
wilaya ya Geita mkoani Geita imemhukumu Joyce Charles(25) mkazi wa mtaa wa
bomani mjini hapa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuiba mtoto Godfrey
Arbet(2) aliyekuwa amemsubiri mama yake nje ya geti kwa ajili ya kwenda
kanisani siku ya krismas mwaka jana.
Hakimu wa
mahakama hiyo Zabron Kesase alielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo siku ya
tar25 desember mwaka jana mnamo saa 4 asubuhi katika mtaa wa ihayabuyaga mjini
hapa ambapom mama huyo wa mtoto aliyekuwa anajiandaa kwenda kanisani na mtoto
wake mara baada ya kumaliza kumuandaa na ili waondoke ghafla alitokea mama huyo
na kumbeba na kuenda nae hadi eneo la mtaa wa kagera kabla hajakamatwa na
wananchi.
Mwendesha
mashitaka wa serikali Fredi Jairo alidai mahakamani kuwa mtuhumiwa siku ya
tukio hilo alimuiba mtoto huyo na kutokomea kusikojulikana huku akidai kuwa
mtoto alimlilia ndio maana akamchukua na kuenda naye na hata hivyo baada ya
mama wa mtoto kubaini kuwa ameibiwa mtoto akatoa taarifa sehemu mbalimbali kwa
wananchi na hatimaye kumkamata mtuhumiwa huyo.
Baada ya
kukamatwa alipelekwa kituo cha polisi ambapo baadaye alipelekwa mahakamani kwa
kitendo alichokifanaya ambapo kamanda wa polisi Leonard Paul alithibitisha kwa
tukio hilo kwa ni alifika kwenye eneo la tukio na kujionea mazingira ya mtoto
huyo kibiwa.
Hata hivyo
baada ya kuridhika na ushaidi uliotolewa na upande wa mashitaka mahakama
ilimtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka saba kabla ya kujitetea mbele ya
mahakama na kupunguziwa adhabu ya miaka mitano kwenda jela ili liwe fundisho
kwa watu wengine wenye nia ya kutaka kutenda makosa ya namna hiyo.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin