Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis,
ametetea rekodi ya kanisa hilo katika utatuzi wa suala la unyanyasaji wa
watoto unaofanywa na mapadri.
Katika mahojiano na gazeti moja la Italia, Papa
Francis amesema kuwa hakuna aliyefanya zaidi kutatua swala hilo kuliko
uongozi wa kanisa hilo.
Amesema kuwa kanisa hilo limewajibika katika kuchukua hatua za uwazi, lakini ndio taasisi inayoshambuliwa.
Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulishtumu,
utawala wa Vatican kwa kushindwa kukabiliana na suala la unyanyasaji wa
watoto mbali na kuwaficha wanaotekeleza tendo hilo.
Via>>bbc