Papa Francis akutana na Obama
Rais Obama ameelezea
furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na
kutenda kulingana na injili anayoihubiri.
|
Rais wa Marekani, Barack Obama akiwasiri Vatican kwa ajili ya mazungumzo na Papa Francis kwenye mji wa Vatican jana march 27, 2014.
Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili Vatican
Rais wa Marekani, Barack Obamaakisalimiana na mmoja wa padri Georg Ganswein alipowasili Vatican
Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda
yakajadiliwa katika mkutano huo. Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna
ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na
kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.
Papa Francis amekuwa mstari wa mbele akipigania kubadili sera na mtazamo
wa Kanisa na viongozi duniani kuhusiana na mikakati ya kupunguza
tofauti kubwa baina ya maskini na matajiri duniani. Aidha viongozi hao
wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo nchini Ukraine, na suala la
upatikanaji wa amani Mashariki ya Kati.
Muafaka baina ya mitazamo tata ya wawili hao kuhusiana na
maswala ya utoaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya
jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa. Baada ya
kukutana na papa, Obama ameratibiwa kukutana na rais wa Italia Giorgio
Napolitano mbali na waziri wake mkuu Matteo Renzi.
Obama amezuru Roma baada ya siku tatu ya mazungumzo na viongozi wa
Uholanzi na Umoja wa ulaya huko Brussels ambapo mada kuu ilikuwa ni
taharuki inayokumba eneo zima la Crimea na Ukraine
Picha na Yahoo, Maelezo na BBC Swahili
Social Plugin