Sakata la
diwani wa CCM viti maalumu Bi Zaituni Fundikira katika kata ya Kalangala wilayani
Geita mkoani Geita kukamatwa na kadi 23 feki za chama cha demokrasia na
maendeleo Chadema kwenye mkoba ndani ya nyumba anayoishi zikiwa na sahihi ya
kugushi ya mwanyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe, limechukua sura mpya
baada ya mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema (BAVICHA) kata ya kalangalala
wilayani humo Deogatias Shinyanga kukemea
vikali na kulaani kitendo cha diwani huyo.
Akizungumza
jana kwenye kikao kilichofanyika kwenye viwanja vya Ihayabuyaga mjini Geita kwa
lengo la kutoa tamko kuhusu diwani huyo amesema kitendo alichofanya diwani huyo ni cha kihuni na cha
kudharirisha chama chao hivyo wanalaani na kukemea kitendo hicho.
Shinyanga
amewataka wananchi wa mkoa wa Geita kuachana na siasa za propaganda
uchwara za wana ccm kwani hawana
jipya na wamekuwa wakitumia kadi zao za kugushi na kwenda nazo kwenye mikuatano
yao na kuzitoa wakidai wamepata wanachama wapya huku ukiwa ni uongo mkubwa.
Ameongeza
kuwa japokuwa wamefungua kesi polisi watahakikisha kesi inafika
mahakamani na kuhakikisha yeye kama mwenyekiti wanashinda ili hilo liwe
fundisho kwa viongozi wengine wanaofikiria
kufanya vitendo hivyo vya kugushi sahihi za viongozi.
wananchi
waliongea na mwadishi wa habari hii wamelaani vikali kitendo cha diwani huyo
kukamatwa na kadi huku akidai yeye amepewa na machokola kitendo ambacho kilivuta
sana hisia za wakazi wa Geita wakiwemo wakereketwa wa Chadema.
Wiki
iliyopita diwani wa CCM wa viti maalumu Bi, Zaituni Fundikira wa kata ya
Kalangalala alikamatwa na kadi 23 za chama cha demokrasia na maendeleo
zilizokutwa kwenye mkoba wake huku yeye akidai amepewa na machokoraa
wanaoishi kwenye pagale(nyumba ambayo haijaisha kujengwa.
Na Valence Robert -Geita.
Social Plugin