Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak, amesema data mpya zinaonyesha
kuwa ndege ya nchi hiyo iliyopotea imeangukia kusini mwa Bahari ya Hindi.
Razak amesema taarifa hizo zimeonyesha kuwa eneo la mwisho la ndege
hiyo ilikuwa katikati mwa Bahari ya Hindi, magharibi mwa mji wa Perth,
Australia.
Amesema eneo hilo liko ndani ndani na liko mbali na uwanja
wowote ule wa ndege.
Amesema kulingana na data hizo mpya, ndege
nambari MH 370 iliangukia kusini mwa Bahari ya Hindi. Razak amesema
taarifa zaidi kuhusu data hizo mpya, zitatolewa kesho Jumanne.
via>>dw swahili
Social Plugin