kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa
polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani imesema kuwa mtuhumiwa
alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi,
ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali
iliyosababisha kukosa hewa na kufariki
Tukio
hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya
Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki
marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta
mkoani Mbeya
Mtuhumiwa
wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya
amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo na
chanzo bado hakijafahamika.
Na Edwin Moshi- Njombe
Social Plugin