UMOJA WA MATAIFA WATUA SHINYANGA-FUATILIA HAPA ZIARA YA MAAFISA WA UN LEO SHINYANGA,WAKUTANA NA WANAFUNZI SHULE 10 ZA SEKONDARI,VYUO NA WALIMU, DC SHINYANGA AHUDHURIA WARSHA
Tuesday, March 25, 2014
Aliyesimama ni afisa habari
kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania (UNIC)bi Usia Nkhoma Ledama
akizungumza leo katika katika viwanja vya Mazingira senta mjini Shinyanga kwenye warsha ya siku moja iliyokutanisha shule 10 za sekondari,vyuo na walimu kutoka katika shule na vyuo hivyo vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema umoja wa Mataifa(UN) unalipa
suala la elimu kipaumbele sana kwa wanafunzi hivyo kuwataka wanafunzi kuwa na
malengo katika maisha yao kwa kusoma kwa bidii,kuepuka vishawishi
vinavyopelekea kupata ujauzito wakiwa wanafunzi tena chini ya umri wa miaka
18.Afisa habari huyo pia akatumia fursa hiyo kuwatahadhalisha wanafunzi wa
kike kuepuka ngono kwani kwa mujibu wa
utafiti wao takwimu zinaonesha kuwa vijana wa kike wenye umri wa miaka 15-19
wana uhusiano wa kingono na wanamme wanaowazidi miaka juu zaidi ya umri wao
hivyo kuwepo kwa hatari ya kuambukizwa VVU na mimba za utotoni.Kushoto ni Mwenyekiti wa
taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra
Manjerenga
Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari kama vile Busurwa,Uhuru,Mazinge,Buluba,Chamaguha,Kizumbi, wakimsikiliza Afisa
habari
kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania bi Usia Nkhoma
Ledama ambaye alisema kwa mujibu wa sensa yao mwaka 2012 asilimia 65 ya
Watanzania wote vijana wenye umri wa miaka chini ya 24,lakini pia
asilimia 40 ya vijana wa kike wenye miaka chini ya 18 wanapata mimba za
utotoni na wengine kuolewa katika umri huo.Aliongeza kuwa asilimia 23 ya
vijana umri wa miaka 15-19 wameanza kuzaa na katika umri huo kati ya
vijana wanne basi mmoja anaolewa ama kupata mimba
Wanafunzi wa
vyuo vya VETA,MUCCOBS,Shycom , wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari kama vile Busurwa,Uhuru,Mazinge,Buluba,Chamaguha,Kizumbi,waliohudhuria katika warsha
hiyo ya Umoja wa Mataifa wakimskiliza Afisa habari kutoka UN,ambaye aliwataka kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Umoja
wa mataifa hapa nchini,lakini pia kuwaomba wazazi na walezi wa wanafunzi
kujenga tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuwasaidia ili kuwafanya
wapende elimu ili kufikia malengo ya millenia
Afisa
habari
kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania bi Usia Nkhoma
Ledama alisema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 52 ya vijana wa kike
umri wa miaka 18-14 wameanza kufanya ngono na na asilimia 7 kwa wenye
miaka 15-19 wanafanya ngono na wanamme wanaowazidi umri miaka 10
zaidi,huku vijana wa kiume wakidaiwa kuanza kufanya ngono wakiwa na umri
wa miaka 20,akatumia fursa hiyo kuwataka vijana kuepuka ngono kwani
wakindekeza ngono UKIMWI upo na hawataweza kutimiza ndoto zao
hivyo.Alisema Umoja wa Mataifa haupo tayari kuendelea kuona vijana
hawatimizi malengo yao
Aliyesimama
ni bwana Innocent Mkota mjumbe wa asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania
akizungumzia kuhusu klabu za Umoja wa Mataifa katika shule za sekondari na
vyuoni ambapo alisema miongoni mwa faida ukiwa mwanachama wa klabu hizo ni
kupata taarifa nyingi tena kwa wakati kutoka UN(kuwa karibu na umoja wa
mataifa),kuhudhuria mikutano ya UN,kupata nafasi ya kusaidia jamii lakini pia
kuwajengea uwezo wa aina mbalimbali kama vile kuongea mbele za watu,kuandaa
ripoti,kupata vyeti n.k
Walimu na
wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika
eneo la viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga ambapo maafisa kutoka umoja
wa mataifa walieleza kazi za umoja wa mataifa na wakatumia muda fursa hiyo
kuitaka jamii kubadilika na kuhamasisha jamii kufuata uzazi wa mpango ikiwa ni
pamoja na kuwa tayari kupiga vita suala la vifo vya akina mama wajawazito na
watoto,mimba za utotoni ambapo watoto wa kike milioni 7.5 miaka chini ya 18
wanazaa kila mwaka
Aliyesimama
ni bwana Moses Mongo ambaye ni Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania
kanda ya ziwa (UNA) akizungumza katika warsha eneo la Mazingira Senta mjini
Shinyanga ambapo alisema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1964 kote duniani na ndiyo
taasisi pekee hapa nchini yenye klabu nyingi yenye lengo la kuwaunganisha watu
wa chini na umoja wa mataifa.Alisema hivi karibuni wamefungua tawi la taasisi
hiyo mkoani Shinyanga na mwenyeki wake ni bwana Ezra Manjerenga.Moses Mongo alitumia fursa hiyo pia kuwataka wanafunzi na wanajamii kwa ujumla kubadilika na kwamba mabadiliko yanaanza kwa kutenda na wafanye kazi kwa malengo ili kuleta mabadiliko katika jamii
Aliyesimama
ni afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania bi Usia
Nkhoma Ledama akizungumza jioni ya leo katika eneo la Mazingira Senta mjini
Shinyanga katika warsha iliyokutanisha shule za sekondari kumi za manispaa ya
Shinyanga lakini pia vyuo mbalimbali kama vile Chuo cha Ualimu cha
Shinyanga,VETA na Chuo cha Ushirika(MUCCOBS),ambapo alieleza kazi mbalimbali za
zinazofanywa na umoja wa mataifa hususani malengo ya millenia kama vile
kuhamasisha afya ya uzazi,haki za binadamu,kupambana na mabadiliko ya tabia
nchi,umaskini,kuhamasisha amani na chakula kwa wenye njaa.Kulia ni mkuu wa
wilaya ya Shinyanga ndugu Anna rose Nyamubi ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Aliyesimama
ni Mwenyekiti wa
taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra
Manjerenga akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Annarose
Nyamubi
katika warsha hiyo iliyokutanisha shule 10 za sekondari na vyuo vitatu
vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga,katikati ni bi Harriet
Macha,ambaye ni mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania,wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna
rose Nyamubi
Mgeni rasmi
katika warsha hiyo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna rose Nyamubi,ambaye ni mdau
wa maendeleo na mwanafamilia wa Umoja wa Mataifa(siku za nyuma aliwahi kufanya
kazi na Umoja wa mataifa katika shirika la UNICEF),alisema nchi ya Tanzania
inatekeleza malengo ya millenia kupitia ilani ya ccm katika kuwaletea maendeleo
wananchi wake hususani katika kupunguza umaskini.Katika hatua nyingine Nyamubi aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa mataifa.Mkuu huyo wa wilaya aliongeza
kuwa serikali inawajali vijana hivyo kuwataka kusoma kwa malengo kwani bila
elimu dunia itawaacha na kuwataka kuacha kutegemea wazazi wao kwamba watarithi
mali.Aidha Nyamubi alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi ambao hawajapeleka
watoto wao kidato cha kwanza wawapeke haraka kabla ya kuwachukulia hatua.
Mapema leo kabla ya warsha-Afisa habari
kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania bi Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha ambapo alisema lengo
la ziara yao ni kuhamasisha uanzishwaji
wa klabu za Umoja wa Mataifa na kutoa elimu kuhusu shughuli za umoja wa mataifa
ambapo huwa wanatembelea shule za msingi,sekondari na vyuo mbalimbali kuwaelimisha
kuhusu ajenda za umoja wa mataifa kama vile changamoto ya mabadiliko ya tabia
nchi, umaskini,ajira,afya ya uzazi,UKIMWI,mimba za utotoni,elimu n.k.
Aliyesimama
ni bwana Moses Mongo ambaye ni Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania
kanda ya ziwa (UNA) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha
iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga,ambapo alisema shuke hiyo ni miongoni mwa
shule chache zilizopata bahati kutembelea na Umoja wa mataifa na kuwataja
miongoni mwa watu ambao ni mazao ya klabu za Umoja wa Mataifa kuwa ni Zitto
Kabwe na John Mnyika.Alisema klabu za Umoja wa Mataifa zinawajengea wanachama
wake ujasiri pamoja na kuwafundisha mambo mbalimbali kama vile elimu ya
ujasiriamali
Wanafunzi
wa Shule ya sekondari Chamaguha wakinyoosha mikono kwamba wako tayari
kuwa na klabu ya Umoja wa mataifa katika shule yao baada ya kuridhishwa
na maelezo kutoka Umoja wa Mataifa hapa nchini wakiongozwa na Afisa habari
kitengo cha habari Umoja wa mataifa Tanzania bi Usia Nkhoma Ledama
Awali katika
shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga,ambako maafisa wa
Umoja wa Mataifa walifanya ziara yao, Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja
wa Mataifa nchini Tanzania bi Harriet Macha akizungumza na wanafunzi wa shule
hiyo ambao wamedhamiria kuanzisha klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule hiyo
ambayo itaundwa na wanafunzi kuanzia 10 na kuendelea.Hapo anaonesha vitabu na
vipeperushi mbalimbali vinavyohusu umoja wa mataifa ambao ulianzishwa mwaka
1945 baada ya vita ya pili ya dunia.Hivi sasa umoja wa mataifa una nchi
wanachama 193 duniani kote na nchi 3 pekee siyo nchi wanachama wa Umoja
huo,nchi hizo ni Taiwan,Cossovo na Vatican
Ni katika
ofisi ya walimu katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya
Shinyanga,muda mchache tu baada ya maafisa kutoka Umoja wa mataifa kuwasili
katika shule hiyo kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.Aliyesimama ni
kaimu mkuu wa shule hiyo bwana Malongo Maganga akiwakaribisha wageni hao ambapo
aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuwafikia na kufurahishwa na mpango wake
kuhusu elimu ya uzazi wa mpango kwa wanafunzi kwani itawasaidia kuongeza uelewa
na kujilinda zaidi ili kutimiza malengo yao.Alisema jamii inaamini kuwa elimu
hiyo ni kwa ajili ya akina mama pekee.Aidha mwalimu Maganga alisema tayari
shule yake imefungua faili kwa ajili ya klabu ya Umoja wa Mataifa kwa wanafunzi
wa shule hiyo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin