Mtoto Said Joshua enzi za uhai wake akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kabla ya kupelekwa Bugando jijini Mwanza baada ya kukatwa koromeo na Baba yake |
Huzuni kubwa imetanda baada ya mtoto Said Joshua (12)
aliyekatwa koromeo kwa kutumia kisu na baba
yake aitwaye Joshua Salvatory (37),usiku wa kuamkia tarehe 4 mwezi huu katika
kitongoji cha Majengo Kaskazini,kata ya Majengo,wilayani Kahama mkoani
Shinyanga ,kufariki dunia jana jioni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali
ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Makula Museven ameimbia www.malunde1.blogspot.com kuwa mtoto huyo alifariki dunia akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama alikokuwa anapatiwa kutokana na koromeo lake kukatwa lote kwa kisu na baba yake kutokana na kile kilichodaiwa kuchoka kumtibu maradhi yaliyokuwa yanamsumbua mara kwa mara.
Kitendo cha kuchinjwa kwa mtoto Said Joshua na hatimaye
kusababisha kifo chake kimeibua mambo mengi huku baadhi ya wakazi wa Kahama
wakidai kuwa pengine kitendo hicho kinatokana na imani za kishirikina kwa madai
kuwa mtuhumiwa alikuwa amemtoa sadaka mwanae kwa waganga ili kupata utajiri na
kwamba Salvatory amefanya kitendo hicho kwa lengo la kulipa mchango wa
Freemason huku wengine wakidai kuwa alitaka kuchangia damu ya mtoto mdogo
akakataliwa.
“Katika miaka kama minne/mitano iliyopita mtuhumiwa alikuwa tajiri,na utajiri huo inasemekana
ulitokana na kumtoa ndagu mtoto wake,akaharibu akili ya mtoto,kila mwezi mtoto
akawa anaanguka kifafa, inasemekana alikiuka masharti ya mganga wake pesa
zikamwishia na mtoto wake akaendelea kubaki katika hali ya kuugua mara kwa mara
ikiwemo kuanguka kifafa kila mwezi”alisema Museven
Mwenyekiti huyo wakitongoji amefafanua kuwa kabla ya
kumkata koromeo mwanaye pia mwezi Julai mwaka jana Salvatory alitaka kumchinja
mke wake Mariam Idd lakini yeye (Museven) akawasuruhisha na mke wa mtuhumiwa
kuamua kumkimbia mme wake kwa hofu ya kuuawa na mwanamme kubaki na mtoto Said
Joshua.
“Siku chache tu
baada ya kuwasuruhisha Salvatory alitaka kumchinja pia mtoto wa jirani yake kwa madai ya kwanini huwa
anacheza na mwanaye ,nikaingilia kati kitendo hicho kilimuudhi Salvatory na
kutaka kunichinja pia,nikaita polisi akakamatwa,na ndiyo tuhuma iliyompeleka
gerezani kwa kipindi cha miezi miwili,”,alieeleza Museven.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Mariamu Idd (35) alisema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio na kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa alikwisha achana na mwanamme huyo siku nyingi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist
Mangalla kwa vyombo vya habari ya tarehe 5,mwezi Machi 2014,alisema chanzo cha
tukio hilo inasadikiwa chanzo cha tukio hilo kinasaikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua
ugonjwa wa akili.
Akizungumza na www.malunde1. blogspot.com mapema leo kamanda Mangalla
amesema kinachofuatia sasa ni mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma
za mauaji zinazomkabili.