VURUGU ZATOKEA SHINYANGA,NAIBU WAZIRI WA MADINI STEPHEN MASELE APIGWA MABOMU WAKATI WA MCHEZO KATI YA STAND UNITED NA POLISI MARA

 
Katika hali isiyo ya kawaida jioni hii kumetokea vurugu katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mchezo kati ya Timu ya Stand United ya Shinyanga na Polisi ya mkoani Mara ambapo wenyeji wa mchezo huo Stand United waliibuka washindi kwa bao moja dhidi ya Polisi.

  Walioshuhudia tukio hilo wamesema vurugu hizo zimetokea mara baada ya mchezo kuisha,ambapo wachezaji wa timu ya Polisi Mara walipotoka uwanjani walimfuata refa wa mchezo huo pamoja na wasaidizi wake kutaka kumpa kichapo,na kufuatia hali hiyo baadhi ya watu waliokuwa katika eneo hilo wakiwemo wachezaji wa timu ya Stand united waliingia uwanjani kutaka kumsaidia refa ili asipigwe.

 Kati ya watu walioingia uwanjani hapo,aliyekuwa mbele alikamatwa na askari polisi waliokuwa eneo hilo na ndipo vurugu zikaanza na askari hao wanaosemekana kuwasaidia POLISI WENZAO wakaanza kurusha mabomu ya machozi katika eneo la jukwaa kuu ambako alikuwepo pia mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini hapa nchini.


Kufuatia vurugu hizo baadhi ya watu waliokuwa eneo la jukwaa kuu akiwemo mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini wamejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za miili yao kutokana na  purukushani za hapa na pale mabomu hayo ya machozi kwani wengine walikuwa wanaanguka hovyo.

 Akizungumza mara baada ya vurugu hizo naibu waziri wa madini Stephen Masele amesema vurugu hizo zimetokana na askari polisi waliokuwa wanawasaidia polisi wenzao yaani timu ya Polisi,walioshindwa kumdhibiti kijana aliyekuwa anakwenda kumsaidia refa.

Masele amesema ni vyema TFF ikaaangalia namna ya kupunguza timu za polisi kwani ziko nyingi sana na wanalindana matokeo yake kusababisha vurugu leo mjini Shinyanga 

BONYEZA HAPA UONE HALI ILIVYOKUWA UWANJA WA CCM KAMBARAGE MJINI SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post