Watu wawili
wamekufa na watatu kuokolewa katika machimbo ya wachimbaji wadogowadogo mchanga yaliyoko katika kijiji cha Mponvu
wilayani Geita baada ya kufukiwa na udongo ndani ya shimo.
Tukio
hilo limetokea Machi 9 mwaka huu majira saa 6 usiku ambapo watu
watano walipanda katika mlima wa Samina na kuanza kuchimba mara ghafla
udongo uliporomoka na
kuwaponda waliokuwemo ndani ya shimo hilo.
Waliopondwa na udongo ni Ngambi Makula(32) mkazi wa Nyarugusu,Juma Makoye(36) mkazi wa Bomani
na waliookolewa ni Mabela Maduhu(31) mkazi wa Mpomvu,Harji Zacharia(26) mkazi wa Nyarugusu,Salama Magangu (26) mkazi wa Busanda.
Mganga
wa zamu wa hospitali ya wilaya ya Geita Dk,George Rweyemela
amethibitisha kupokea miili miwili ya marehemu na majeruhi watatu ambao
wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku miili ya marehemu
iliyokuwa imehifadhiwa chumba cha maiti imeshatambuliwa na ndugu zao na
wameshaichukua kwa mazishi.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul
amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na amesema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa na amewaasa
vijana kutoenda maeneo hatari ambayo yanaweza kusababisha maafa wakati
taifa bado linawahitaji kulitumikia,alisema kamanda huyo kwa uchungu wa
tukio hilo.
Tukio hili limetokea siku chache tu
baada ya watu wawili kukaa ndani ya shimo kwa siku 4 kisha kuokolewa wakiwa
hai katika machimbo ya mgodi wa GGM eneo la Kukuluma mkoani Geita.
Na Valence Robert-Geita