Kituo cha afya cha
Ikonongo kilichopo kata ya Salawe
wilayani Shinyanga kinakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo
ukosefu wa huduma ya maji na nishati ya umeme hali ambayo inawalazimu akina mama wajawazito kutumia tochi ya simu au taa wakati wa kujifungua huku
watoto wanaougua kuchanganywa na wakubwa.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo walieleza kuwa
kumekuwepo na tatizo la kupata huduma iliyo bora kwani vifaa vya kupimia maradhi yanayowasumbua
hakuna, mama wajawazito kutumia mwanga
wa simu ya tochi wakati wa kujifungua , wamalizapo kujifungua nguo zao hulazimika kwenda kufulia kwenye malambo sehemu ambayo maji hutumiwa na watu wote.
Walisema
wamekuwa wakipata shida ya kupata
huduma katika kituo hicho kwani
hakuna maji hivyo wanapokwenda kujifungua hulazimika kwenda
na maji yao.
Mwenyekiti wa kijiji cha
Azimio Twiga Mashimba
alisema kuwa kituo hicho
kinahudumia vijiji zaidi ya vitano na kata nne ambazo ni Mwakitolyo,Mwenge na Salawe ambapo kijiji chake kina watu zaidi ya 3000
na kwamba kituo kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wodi ya watoto
ambao hulazimika kuchanganywa na
wakubwa, kina mama hujifungua kwa kutumia mwanga wa simu ya tochi pia uhaba wa
maji upo.
“ Kijiji hiki kinahudumia zaidi
ya watu 21,000, awali kulikuwepo na sola ambayo ilikuwa ikisaidia kurahisisha huduma mbalimbali kwa wagonjwa
lakini ilikwisha ibiwa na sasa hakuna sola vifaa vya kupimia maradhi mbalimbali ikiwemo malaria hakuna
,wodi ya kulaza watoto hakuna
inawalazimu kuwachanganya na wakubwa hata
wenye magonjwa ya kifua kikuu na kuhara”alisema .
Naye mkuu wa kituo
hicho Dkt Saimon Wilson alisema vifaa vya kupimia baadhi ya maradhi
vipo ila kuna wengine wagonjwa hulazimisha kupata vipimo vyote vingine havipo ila kwa
upande wa kupima malaria kipimo kipo,
suala la kujifungulia tochi ya simu sio
kweli bali wanatumia taa ikiwa sola iliyopo haina nguvu na huzimishwa
ifikapo saa tano usiku.
"Kituo hiki
kinakabiliwa na changamto ya maji
na nishati ya umeme, suala la sola
kuibiwa siwezi kulizungumzia mimi
nilikuta sola iliyopo na inatumika mpaka sasa ni hii nayo haina nguvu
huwashwa na kuzimishwa saa tano usiku ,tunatumia
taa za kawaida,pia wagonjwa kwa siku ni zaidi ya 80",aliongeza.
Diwani wa kata hiyo
Joseph Budonho alisema kuwa kweli
kituo hicho cha afya
kina changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme na maji ila tatizo hilo linashughulikiwa ikiwa tayari nyaya za umeme zimekwisha wekwa isitoshe kuondoa tatizo la maji lililopo, kuhusu sola ilikuwepo
zamani lakini iliibiwa na kesi bado ipo mahakamani.
Chanzo-Kareny Blog