Sekta ya
elimu hapa nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi,ambapo huko mkoani Simiyu wanafunzi 1302 katika
shule ya msingi Kidinda iliyopo kata ya Bariadi katika halmashauri ya Mji wa
Bariadi wanakaa chini kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa
madawati kwa muda mrefu.
Shule hiyo
ina jumla ya wanafunzi 1622, wavulana wakiwa 807 na wasichana 815, mbali na
kukabiliwa na upungufu huo wa madawati, bado madarasa ni machache hali inayosababisha
zaidi ya wanafunzi 200 kujazana ndani ya chumba kimoja cha darasa.
Mwalimu mkuu
wa shule hiyo Josephina Sitta amesema kutokana na changamoto hizo shule yake ina
jumla ya madawati 190 na kila dawati linakaliwa na wanafunzi 3, ambapo wanafunzi
570 ndiyo wanaokaa kwenye madawati, na wanafunzi 1302 wakiwa wanakaa chini hali
inayosababisha kuwepo kwa upungufu wa madati 434.
Amesema
kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi kila mwaka katika shule yake imesababisha shule hiyo inahitaji
jumla ya vyumba vya madarsa 6, na sasa vyumba vya madarsa viko 11 hali
inayopelekea darasa moja kutumiwa na wanafunzi zaidi ya 200.