Kampuni ya Microsoft, inayojishughulisha na utengenezaji wa kompyuta pamoja na programu, imebuni mbinu mpya ya kukabiliana na wizi wa mitandaoni ambao umezisababishia hasara benki, kampuni na watu binafsi katika maeneo mengi duniani.
Mkakati huo umekuja wakati benki nyingi nchini
zikiathiriwa na wizi huo kupitia mashine za kutolea fedha maarufu kama
ATM pamoja na miamala inayofanyika kupitia mifumo ya mawasiliano ya
kompyuta.
Takwimu zinaonyesha katika kipindi cha Oktoba 2012
hadi Februari 2013, Tanzania inakadiriwa kuwa Sh700 milioni ziliibwa
katika benki kwa nyakati tofauti.
Kutokana na hali hiyo Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania, Profesa Benno Ndulu aliziagiza taasisi za fedha kuchukua hatua
ili kukabilina na hali hiyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Microsoft, David Finn imeeleza kuwa
wamebuni kompyuta mpya pamoja na programu ambazo zinaziba mianya ya
wizi.
Imeweka wazi kuwa uuzaji holela wa programu za kompyuta duniani umekuwa chanzo cha wezi hao kutumia ujanja katika kufahamu taarifa za siri zilizohifadhiwa kwenye kompyuta za taasisi na hata watu binafsi zilizounganishwa kwenye mtandao.
Imeweka wazi kuwa uuzaji holela wa programu za kompyuta duniani umekuwa chanzo cha wezi hao kutumia ujanja katika kufahamu taarifa za siri zilizohifadhiwa kwenye kompyuta za taasisi na hata watu binafsi zilizounganishwa kwenye mtandao.
“Kampuni na taasisi na Serikali zinashauriwa
kununua kompyuta mpya kwa mawakala maalumu zitakazowekewa ‘software’
(programu) zilizo halali,” alisema Finn na kuongeza:
“Utafiti uliotolewa mwaka huu na kampuni ya
kimataifa ya teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ikishirikiana na Chuo
Kikuu cha Singapore unaonyesha, wizi wa kwenye mtandao unagharimu
kampuni zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 315 kwa mwaka sawa na Sh504
trilioni,”.
Sehemu ya ripoti hiyo imeeleza kuwa maeneo mengi
ya Afrika yanakua kwa kasi katika matumizi ya mitandao kutokana na
vitendo vya kiharamia na wengi wamejikuta wakipata hasara kwa kuibiwa
fedha zao.
“Wizi wa njia ya mtandao unahamasishwa na tamaa ya
pesa bila jasho kwa kutumia werevu wa teknolojia kuingilia na kuchukua
taarifa muhimu za mtu, kitambulisho, namba za siri au hata pesa, hivyo
Microsoft imedhamiria kudhibiti vitendo hivyo ili kuongeza usalama wa
taarifa za wateja,” alisema Finn.
Anasema utafiti umebaini kuwa kompyuta 203 zilizo
nunuliwa katika maduka 11 tofauti, zilibainika kuwa asilimia 61
ziliathiriwa na programu za kiwizi maarufu kama virusi vinavyoitwa
trojans, worms, viruses, hacktools, rootkits na adware.
Social Plugin