Mkazi wa kijiji cha Ilindi wilayani Kilolo Thomas Kilonge(42), amefariki dunia baada ya kung’atwa na nyoka.
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo limetokea juzi kijijini hapo na kumtaja aliyefariki kuwa ni mkulima wa kijiji cha Ilindi.
Hata hivyo alidai kuwa mazingira ya kung’atwa na mdudu huyo bado hayajajulikana na kwamba, jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wake.
NA FRANK KIBIKI, IRINGA
Social Plugin