Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AKUTWA PORINI AKIWA AMEKUFA BAADA YA KUPIGWA MAWE NA FIMBO-SHINYANGA

Kamanda  wa polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla
Mwanamme mmoja asiyejulikana jina wala makazi yake amekutwa amekufa kwa kupigwa mawe na fimbo,katika pori la Mwaweja lililopo katika kijiji ch Mwaweja,kata ya Ukenyenge,tarafa ya Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa SACP Evarist mangalla amesema tukio hilo limetokea  jana majira saa saba mchana ambapo mwanamme huyo asiyejulikana jina,kabila wala makazi yake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 30.

Kamanda Mangalla amesema hivi sasa jeshi la polisi linaendelea na msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wahusika  wa mauaji hayo huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com