Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla |
Mwanamme mmoja asiyejulikana jina wala makazi yake amekutwa
amekufa kwa kupigwa mawe na fimbo,katika pori la Mwaweja lililopo katika kijiji
ch Mwaweja,kata ya Ukenyenge,tarafa ya Negezi wilayani Kishapu mkoani
Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa SACP Evarist mangalla amesema
tukio hilo limetokea jana majira saa
saba mchana ambapo mwanamme huyo asiyejulikana jina,kabila wala makazi yake
mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 30.
Kamanda Mangalla amesema hivi sasa jeshi la polisi
linaendelea na msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wahusika wa mauaji hayo huku akiwataka wananchi kutoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.
Social Plugin