Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ama kweli wajinga ndiyo waliwao!! MREMBO ATAPELIWA SIMU 4 NA MGANGA WA KIENYEJI,ETI ASAFISHIWE NYOTA

Wanawake watatu wasiojulikana majina yao wamemtapeli mwanafunzi wa Chuo cha Jiji la Dar es salaam (Dacico), Monica Crispin simu nne zenye thamani ya Sh145,000 baada ya kumdanganya kwamba watamsaidia kusafisha nyota ili fanikiwe katika maisha yake.

Mwanafunzi huyo alisema kwamba alikutana na matapeli hao karibu na lango la chuo na mmoja wao alimwomba aelekezwe kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Mama John.
Monica alisema alimjibu kwamba hamfahamu na ghafla alijitokeza mwanamke wa pili aliyejifanya anamfahamu Mama John na kumtaka Monica aongozane nao ili akawaonyeshe.
Alisema alikubali kuwaongoza, lakini baada ya dakika chache mmoja wao alimwambia kuwa wao ni wasafisha nyota na wanataka kumsaidia. “Walinitaka niwapatie kiasi chochote cha fedha, lakini nilipowaambia kwamba sina, wakanishauri niwape simu hata kama ni nne au zaidi ili wazisafishe nyota,” alisema.
Monica alisema katika mazingira ambayo hakumbuki, alijikuta akikubali kila kitu na hatimaye alikwenda darasani kuwaomba wanafunzi wenzake wampe simu ambazo alizipeleka kwa wanawake hao.
Alisema aliwapelekea simu wanawake hao na baada ya kupata simu hizo walimtoroka.
Baada ya kutapeliwa alikwenda moja kwa moja nyumbani ambako alimweleza mama yake ambaye alifika naye shuleni na kuwalipa wanafunzi wote waliokuwa wakimdai simu mwanafunzi huyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com