Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMA KWELI WILAYA YA KISHAPU WAMEDHAMIRIA KUPAMBANA NA NJAA,VIONGOZI WAONESHA MFANO KULIMA MTAMA,TAZAMA HAPA

Ni katika ziara ya siku moja ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mgeja wilayani kishapu,akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa siasa ya mkoa, iliyolenga kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM hususani katika sekta ya kilimo ambapo pia alikagua shamba la mtama la mfano lililolimwa na katibu wa CCM wilaya ya Kishapu bi Khadija Kasola Kusaga katika kijiji cha Sulagi kata ya Uchunga.

Pichani ni viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa mkoa wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(mwenye kofia hapo mbele) pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kishapu mkoa wa  Shinyanga wakiwa katika shamba darasa la mtama katika halmshauri ya wilaya ya Kishapu lililolimwa na katibu wa ccm wilaya hiyo bi Khadija Kasola Kusaga (wa pili kutoka kushoto)
Viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiwa katika shamba la mtama katika kijiji cha Sulagi kata ya Uchunga,ambalo lipo kama mfano kwa wananchi wilayani humo.Mkoa wa Shinyanga umejiwekea utaratibu wa kila kaya kulima hekali mbili za mtama ili kukabiliana na baa la njaa mkoani humo na wilaya ya Kishapu imepongezwa na uongozi wa ccm mkoa wa Shinyanga kwa kuwa mstari wa mbele katika suala hilo ambapo viongozi wake kuanzia ngazi za chini wanalima mtama likiwa ni miongoni mwa mazao yanayostahimili ukame.
Akiyeko mbele ni katibu wa ccm wilaya ya Kishapu bi Khadija Kasola Kusaga akimwonesha mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga zao la mtama shambani kwake,wakati wa ziara yake wilayani humo kukagua utekelezaji wa ilani ya chama tawala hususani katika sekta ya kilimo ambapo pamoja na mambo mengine mwenyekiti huyo wa ccm mkoa wa Shinyanga aliwataka viongozi wa chama na serikali kuwa mstari wa mbele kutekeleza wanachokiongea majukwaani ili wananchi wajifunze kutoka kwa viongozi wao,huku akitoa pongezi kwa halmashauri ya Kishapu kwa jitihada zake katika kupiga vita janga la njaa wilayani humo na kuzitaka halmashauri zingine kuiga mfano huo

Katikati mwenye suti ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwa na viongozi wa chama cha mapinduzi wakitembelea shamba la mtama lenye hekali 11 zilizolimwa mtama,zikiwa ni juhudi za katibu wa ccm wilaya ya Kishapu,ambaye mbali na kulima hekali za mtama 11,akitumia mbegu iitwayo  masiha wengine huiita Ndala saba pia amelima hekali 3 za karanga,5 za mahindi na choroko hekali 2 katika eneo la kijiji cha Sulagi kata ya Uchunga wilayani humo.

Msafara wa mwenyekiti  wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ukitoka katika eneo la shamba darasa la mtama wilayani Kishapu,katika msafara huo yumo pia katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Shinyanga ndugu Emmanuel Mlimandago(wa pili kutoka mbele),yumo MNEC Boniface Butondo(wa tatu kutoka mbele),afisa habari wilaya ya Kishapu ndugu John Mlyambate(wa pili kutoka kushoto)

Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga bi Khadija  Kasola Kusaga akiwa katika shamba lake la mtama lililopo katika kijiji cha Sulagi kata ya Uchunga wilayani humo.Mtama ni miongoni mwa mazao yanayostahimili ukame ambapo mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kulipa kipaumbele zao hilo ili kuondoa adui njaa kwani ni aibu kwa mkoa kila mara kutembeza bakuli kuomba chakula na kuongeza kuwa kama nchi inajitosheleza kwa chakula hata amani inakuwepo na kwamba kama wananchi wana njaa hata siasa haiwezi kufanyika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com