Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZAM FC WAICHAPA MBEYA CITY BAO 2 KWA 1 UWANJA WA SOKOINE,NI RASMI SASA AZAM NDIO BINGWA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA

AZAM_FC_PLAYERS
AZAM FC Leo huko Uwanja wa Sokoine, Mbeya, wamevunja ule mwiko wa kutotwaa Ubingwa kwa Klabu nyingine mbali ya Yanga na Simba wa tangu Mwaka 2000 baada ya kuichapa Mbeya City Bao 2-1 katika Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom.

Kwa kutwaa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 1 mkononi, Azam FC imefuta kuhodhi kwa Ubingwa kwa Vigogo Yanga na Simba tangu Mwaka 2001 ambapo, baada ya Mtibwa kuutwaa Mwaka 2000 na kuutetea Mwaka 2001, Yanga na Simba zimekuwa zikipishana kwa kuubeba.

MSIMAMO-Timu za Juu:

NA TIMU P W D L GD GF PTS
1 Azam FC 25 17 8 0 35 50 59
2 Yanga SC 25 16 7 2 42 60 55
3 Mbeya City 25 12 10 3 12 31 46
4 Simba SC 25 9 10 6 14 40 37



Katika Mechi nyingine zilizochezwa Leo, Yanga waliichapa JKT Oljoro Bao 2-1 hukO Arusha na Jijini Dar es Salaam, Simba ilitunguliwa Bao 1-0 na Ashanti United.

 VPL itakamilika Wikiendi ijayo Aprili 19 kwa Timu zote 14 kuwa Dimbani.

RATIBA/MATOKEO:

Jumapili Aprili 13

Simba 0 Ashanti United 1 (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)

Mbeya City 1 Azam 2 (Sokoine, Mbeya)

JKT Oljoro 1 Yanga 2 (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Mgambo Shooting 0 Kagera Sugar 0 (Mkwakwani, Tanga),

Mtibwa Sugar 0  Ruvu Shooting 1 (Manungu, Morogoro),

MABINGWA WALIOPITA:

1965 Sunderland (Sasa ni Simba SC)

1966 Sunderland

1967 Cosmopolitan

1968 Young Africans

1969 Young Africans

1970 Young Africans

1971 Young Africans

1972 Young Africans

1973 Simba SC

1974 Young Africans

1975 Mseto SC

1976 Simba SC

1977 Simba SC

1978 Simba SC

1979 Simba SC

1980 Simba SC

1981 Young Africans

1982 Pan Africans

1983 Young Africans

1984 Simba SC

1985 Young Africans

1986 Tukuyu Stars

1987 Young Africans

1988 Coastal Union

1989 Young Africans

1990 Simba SC

1991 Young Africans

1992 Young Africans

1993 Young Africans

1994 Simba SC

1995 Simba SC

1996 Young Africans

1997 Young Africans

1998 Young Africans

1999 Mtibwa Sugar

2000 Mtibwa Sugar

2001 Simba SC

2002 Young Africans

2003 Simba SC

2004 Simba SC

2005 Young Africans

2006 Young Africans

2007 Simba SC

2007/08 Young Africans

2008/09 Young Africans

2009/2010 Simba SC

2010/2011 Young Africans

2011/2012 Simba SC

2012/2013 Young Africans

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com