Kaya zaidi
65 hazina mahali pa kuishi katika kijiji cha Kabondo kata ya Mwanase Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga baada ya nyumba zao kusombwa na Mvua
kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kijiji hicho juzi
na kusababisha hasara kubwa ya mali kwa wakazi hao.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabondo Elias Paul
alisema kuwa Mvua hiyo iliyokuwa ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali ilianza kunyesha majira ya saa nane za usiku na
hivyo kusababisha maafa hayo makubwa.
Paul alisema kuwa mbali na uharibifu huo wa nyumba
mvua hiyo pia imezoa mazao yalikuwa yamelimwa yakiwemo mpunga, na Wakulima
katika kijiji hicho hali ambayo inafanya Wananchi hao wahitaji msaada wa haraka
ili kuwanusuru tatizo na tatizo la njaa
linaweza kutokea kwa kipindi hiki.
Aidha Mtendaji huyo akiongea na Waandishi wa habari
aliendelea kusema kuwa kutokakana na uharibifu huo mkubwa ambao pia
umesababisha mazao kama yale ya Mpunga aliyokuwa shambani kwenda na maji hali
ambayo inaweza kusababisha upungufu mkubwa chakula katika kata hiyo.
Hata hivyo Mtendaji huyo aliendelea kusema kuwa
wananchi nyumba zao zilizochukuliwa na maji kwa sasa wamehifadhiwa na majirani
zao huku wakisubiri msaada wowote kutoka katika ofisi ya ya Mkuu wa Wilaya ya
Kahama ili waweze kumudu maisha yao.
“Kwa sasa ndugu Mwaandishi wa habari hata usafiri wa
kutoka katika kijiji hicho kuja mjini Kahama ni Mgumu kwani barabara hazipitiki
unatumia muda wa masaa hata saba kutoka katika sehemu husika ambayo ni karibu
kabisa na Mjini”, Alisema Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabondo Aliasi Paul
Aidha alisema msaada kama vile wa
Mahema kwa wahanga hao unahitajika kwani kwa sasa sehemu walipojishikiza
wamekuwa wakiishi zaidi ya watu 14 huku wengine wakikaa katika majiko ili
kujisitiri wao na watoto hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.
Katika Wilaya ya Kahama kuna uwezekano mkubwa wa
wananchi kuendelea kuathirika na mvua za masika zinazoendelea kutokana na baadhi
ya wananchi wengi hasa katika maeneo ya Vijijini kutokuwa na nyumba imara
ambazo inaweza kuhilimi mvua hizo.
via Raymond Mihayo blog
Social Plugin