MAHUSINO baina ya Kampuni ya African Barrick Gold Mines Ltd
inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama uliokuwa
umetetereka na kuzua migogoro na jamii inayozunguka mgodi yanazidi
kuimarika kutokana ma mabadiliko ya uongozi wa Idara ya Mahusiano ya
Jamii.
Hayo yalibainishwa juzi na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Ramadhani
Madese, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini mwake na kudai
hali ya sasa hivi ni shwari kutokana na idara ya mahusiano ya mgodi huo
kukaa na wananchi kwa maelewano jinsi ya kumaliza kero zinazojitokeza.
Alieleza awali idara ya mahusino ilikuwa na mapungufu makubwa
kutokana na maamuzi yake kuyafanya kibabe, hali iliyozua migogoro ya
mara kwa mara na wananchi ambao wakati mwingine walikuwa wakiziba
barabara kuzuia magari na shughuli za mgodi zisifanyike.
Hata hivyo, alisema kwa kipindi hiki idara hiyo ya mahusiano
inayoongozwa na Meneja wake, Abdallah Msika, aliyewahi kuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga imekuwa na mahusiano mazuri kiasi cha kumudu
kufanya marekebisho makubwa kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo, hali
iliyofanya kuimarisha usalama eneo la mgodi.
Na
Ali Lityawi-Kahama
Social Plugin