Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BARRICK WAIMARISHA MAHUSIANO NA JAMII HUKO KAHAMA

 
MAHUSINO baina ya Kampuni ya African Barrick Gold Mines Ltd inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama uliokuwa umetetereka na kuzua migogoro na jamii inayozunguka mgodi yanazidi kuimarika kutokana ma mabadiliko ya uongozi wa Idara ya Mahusiano ya Jamii.


Hayo yalibainishwa juzi na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Ramadhani Madese, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini mwake  na kudai hali ya sasa hivi ni shwari kutokana na idara ya mahusiano ya mgodi huo kukaa na wananchi kwa maelewano jinsi ya kumaliza kero zinazojitokeza.

Alieleza awali idara ya mahusino ilikuwa na mapungufu makubwa kutokana na maamuzi yake kuyafanya kibabe, hali iliyozua migogoro ya mara kwa mara na wananchi ambao wakati mwingine walikuwa wakiziba barabara kuzuia magari na shughuli za mgodi zisifanyike.

Hata hivyo, alisema kwa kipindi hiki idara hiyo ya mahusiano inayoongozwa na Meneja wake, Abdallah Msika, aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imekuwa na mahusiano mazuri kiasi cha kumudu kufanya marekebisho makubwa kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo, hali iliyofanya kuimarisha usalama eneo la mgodi.
Na Ali Lityawi-Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com