Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za
msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Muhidini
Maalimu Ngurumo
“ Baraza
limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha
Muhidini Maalimu Ngurumo ambaye mchango wake katika muziki wa dansi ni
mkubwa mno na unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani
ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.”
Baraza
linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha
tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na
mpendwa wetu.
Mwenyezi
Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja
na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Imetolewa na
Godfrey Mngereza
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.
Social Plugin