Vilio vimetawala miongoni mwa
waumini wa kanisa katoliki jimbo la Geita katika kanisa la Bikira Maria wa
Fatma la mjini Geita kufuatia taarifa
za kifo cha poroko wa parokia ya Geita Padri Henry Kimisha aliyefariki ghafla leo
asubuhi katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuugua ghafla.
Akitoa
taarifa za kifo hicho hilo leo msaidizi wa askofu jimbo la Geita Pdr Nikodema Duba
amesema paroko huyo amefariki dunia saa 2 asubuhi baada ya kuugua ghafla na kulazimika
kumpeleka hospitali ya wilaya ya Geita na wakati wakifanya maandalizi ya kumpeleka
hospital ya mission Sengerema ghafla akakata roho.
Aidha
msaidizi wa askofu huyo amesema paroko huyo alikuwa anasumbuliwa na
shinikizo la damu(presha) hivyo na muda huo hali yake ilibadilika ghafla kiasi
cha kumpeleka hospitali haraka lakini mwenyezi mungu akamchukua.
Baadhi ya
waumini na wasio waumini wa kanisa katoliki wameshtushwa na kifo cha paroko
huyo ambaye wanamfahamu na amekuwa akishirikiana nao katika mambo ya kijamii na
shughuli mbalimbali zilizokuwa zinahusu jamii hiyo.
Naye katibu
wa parokia hiyo Bw,Mansety Kyara amemlilia paroko huyo na kuongeza kuwa
walikuwa katika maandalizi ya kumuaga Baba askofu Damian Dallu aliyehamishiwa
jimbo la Songea mkoani Ruvuma.
Padri
kimisha alizaliwa tarehe 8/6/1967 katika kijiji cha katunguru wilayani
Sengerema mkoani Mwanza na alipata daraja takatifu ya upadri tarehe 25/7/1996 katika
parokia ya nyantakubwa wilayani sengerema na mazishi yake yatafanyika ijumaa
katika makaburi ya kanisa hilo ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hospitali ya rufaa Bugando.
Mungu ailaze mahali pema mbinguni roho ya marehemu Henry Kishima,Amina!!!
Mungu ailaze mahali pema mbinguni roho ya marehemu Henry Kishima,Amina!!!
Na Valence Robert Geita
Social Plugin