Habari zilizoufikia mtandao wa Malunde1 blog hivi punde
kutoka mkoani Simiyu ni kuhusu ajali mbaya ambapo watu zaidi ya 10 wamefariki dunia papo hapo na
wengine wengi kujeruhi baada ya basi la Luhuye walilokuwa wanasafiria kugonga nyumba na kupinduka kutokana na kile kilichotajwa kuwa mwendo kasi wa basi hilo.
Habari zinasema kuwa basi la abiria la kampuni ya Luhuye lenye namba za usajili T 410 AWQ lililokuwa likitokea
Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza limegonga nyumba na kupinduka leo saa tano asubuhi katika
barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Itwilima kata ya Kiloleli wilaya ya
Busega mkoani Simiyu.
Social Plugin