BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA IVUMWE MBEYA LATEKETEA KWA MOTO



Bweni Moja  la Wavulana lenye vyumba zaidi ya  Sita  katika shule ya Wazazi Sekondari ya Ivumwe  inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea leo April 23  majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya   wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Akizungumza katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi wakati tayari wanafunzi wakiwa madarasani.

Amesema taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo.

Amesema mara baada ya kupata habari hizo   walitoa taarifa kwa kikosi cha zimamoto ambacho kilifika mara moja na kuanza juhudi za kuuzima moto huo.

Amesema pamoja na kikosi hicho cha zimamoto kufika shuleni hapo mapema na kuzima moto huo lakini tayari moto huo ulikwisha teketeza asilimia kubwa ya mali zilizomo katika mabwani hayo.

Amesema kwa kiwango kikubwa vitu vingi vimeteketea kwa moto huo   hususani vitanda na magodoro ambayo ndiyo yaliyoungua vibaya  pamoja na vitu vingine vya wanafunzi hao.

Aidha kwa mujibu wa Daktari Kanama hakuna mwanafunzi yoyote aliye poteza maisha kutokana tukio hilo licha ya mmoja wa wanafunzi kujeruhiwa mkononi na kitu kinacho dhaniwa kuwa ni kioo katika harakati za kuokoa vitu ambapo tayari amekwisha fikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga amesema mabweni hayo yalichukua jumla ya wanafunzi 160  ambao ni wavulana huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Amesema  kwa sasa juhudi zinazofanyika na Chama kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo  ili kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwahifadhi wanafunzi hao.

Amesema litatengwa darasa moja kwa muda ambalo litatumika kama bweni wakati wakiendela kufanya utaratibu mwingine.
 

via>>fahari news

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post