Katikati ni ndugu Charles Shigino Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya shinyanga mjini akiwa anahojiwa katika kipindi cha SAUTI YA WATU ndani ya studio ya Radio Faraja FM Stereo ya mjini Shinyanga ambapo katibu huyo anadai yeye binafsi anataka serikali 3 japo sera ya chama chake inataka serikali mbili(Picha na Veroca Natalisi)
Wakati mvutano wa serikali mbili,serikali
tatu,ukiendelea kuchukua sura mpya kila kukicha,Katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya
ya Shinyanga Mjini Charles Shigino ameunga mkono muundo wa serikali tatu na
kueleza kuwa hayo ndiyo maoni ya wananchi walio wengi yaliyopitishwa katika
mchakato wa rasimu ya katiba ambayo iliundwa na tume ya Jaji Warioba.
Akizungumza jana jioni katika kipindi cha Sauti ya watu kinachorushwa na radio faraja Fm stereo
inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Shinyanga, Shigino alisema suala
linalosumbua na kuleta migogoro,migongano na matusi katika mchakato wa kuunda
katiba mpya ni kutokana muingiliano wa sera ya vyama.
Alisema hivi sasa kila chama kinakuwa na
msimamo wake mfano CCM kina msimamo wa serikari mbili, CHADEMA, CUF kinataka
serikari tatu, na kufuatia hali hiyo wafuasi wa vyama hivyo lazima wafuate
msimamo wa vyama vyao suala ambalo linaleta mfarakano
Shigino alidai kuwa yeye binafsi anaunga
mkono muundo wa Serikali tatu lakini kutokana na sera ya chama chake cha mapinduzi
inamlazimu awe muumini wa Serikari mbili.
Akizungumzia kuhusu suala la Umoja wa
katiba ya wananchi (UKAWA) kutoka nje ya bunge na kususia vikao vya
bunge la katiba linaoendelea mkoani Dodoma alidai kuwa wabunge hao wapo sawa
kususia bunge hilo kwani asilimia kubwa ya wabunge waliobaki ndani ya bunge
wamekuwa wakiwanyanyasa wabunge hao kwa kukejeri hoja zao na wakiwazomea
kitendo ambacho amedai ni ukiukwaji wa haki na kanuni za bunge.
Shigino ameonesha msimamo wake wa kutaka
serikali tatu,ikiwa ni siku chache tu baada ya mbunge wa Kahama James
Lembeli kuonesha msimamo wake kuunga mkono serikali tatu hivyo kwenda kinyume na msimamo wa chama
chao kinachotetea na kuamini serikali
mbili.
|
Social Plugin