Wengi hudhani wanawake wengi wanaovaa nguo zinazoonesha sehemu kubwa ya mwili(nusu uchi) huwa wanajiuza. Ukweli ni kuwa hiyo ni sababu mojawapo.
Wanawake wa kundi hili huvaa nguo zinazoonesha mapaja, kuta za matiti, mgongo au kitovu wakiamini huwavutia wanaume na watawatongoza na kufanya biashara yao ya ngono.
Lakini kuna sababu KUU
Sababu ni kuwa wengi huwa wanavaa vijinguo hivyo ili kuficha udhaifu wa maumbile yao.
-Mathalani msichana huyo yeye mwenyewe akadhani na kuamini kuwa ana sura mbaya, hivyo suluhu yake ya kuficha udhaifu huo ni kuvaa nguo zinazoacha sehemu kubwa ya mwili wazi ili kutoa ujumbe kuwa "japo nina sura mbaya lakini miguu, tumbo, au matiti yangu mazuri". Lengo ni kuonesha kuwa japo ana sura mbaya lakini ana sehemu nyingine nzuri na zinazovutia.
-Au labla binti mzuri wa sura na natural color, lakini hajaolewa. Naye anaweza kuvaa nusu uchi ili kuleta ujumbe kuwa "japo sijaolewa lakini mimi ni mzuri wa sura na viungo vyangu vingine" ili tu kuwavutia wanaume aidha wasione udhaifu wake wa kutoolewa na/au atongozwe.
-Kuna kundi la mwisho wao huvaa nusu uchi kwa vile tu labla anaona rafiki zake wanavaa nguo fupi na wanaambizana wanapendeza. Mfano: binti yuko chuo na akaona wenzio wanavaa nguo fupi na kila mmoja wao akivaa nguo fupi anaambiwa "UMEPENDEZA" hakika hapo binti hujikuta anatafuta vijinguo vya ajabu ili afanane na wenzio "waliopendeza".
Watu hudhani kuwa mavazi huwasilisha tabia. Mfano binti akivaa nusu uchi basi huwa malaya, ukweli ni kuwa mabinti wengi huamini kwa kuvaa nusu uchi watakuwa wameficha udhaifu wao na watakuwa wametoa ujumbe kuwa "kama sina sura nina hiki kizuri".
Chukulia utafiti wa haraka mabinti wengi wenye makalio makubwa huwa na watu huamini wana sura mbaya, kwa kuonesha kuwa wao hawajakosa vyote huvaa suruali za kubana au sketi fupi ili "shughuli" ionekane nyuma
Social Plugin