|
Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwa katika ziara yake
katika kijiji cha Mwamashimba kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu kukagua utekelezaji
wa ilani ya CCM,hapoa ni katika mradi wa maji yanatokana na mto uliopo katika
eneo hilo akimtwisha ndoo ya maji mwanamke aitwaye Rahel Daudi mkazi wa kijiji cha
Mwamashimba ikiwa ni ishara ya mradi huo kuanza kutumika rasmi
|
|
Diwani wa kata ya Mwamalasa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Justine Sheka awali akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji ch Mwamashimba ambapo pamoja na mambo mengine alisema wilaya hiyo inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na sasa jumla ya shilingi milioni 100 zimetengwa kwa ajili ya kuanzisha kituo cha radio katika wilaya hiyo kitaachoitwa Radio Kishapu inayotarajiwa kuanzishwa mwezi Julai mwaka huu |
Diwani wa kata ya Mwamalasa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Justine Sheka akiwatambulisha baadhi ya wataalam kutoka katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
|
Wakazi wa kijiji cha Mwamashimba wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika eneo la mkutano
|
Burudani inaendelea katika eneo la mkutano,kwaya maarufu kwa jina la Sauti ya Nyikani kutoka kijiji cha Mwamashimba ikitumbuiza mkutano wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho,kikundi hicho baada ya burudani kilipewa shilingi elfu 75 na msafara wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga,lakini pia vijana wake kwa waume katika kijiji hicho wakapatiwa mipira kwa ajili ya michezo ya netbali na mpira wa miguu |
|
|
Mkutano unaendelea,wananchi na viongozi wa chama wakifurahia burudani katika eneo la mkutano |
|
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kishapu Shija Malisha Nteleju akimkaribisha mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ili azungumze na wananchi wa kijiji cha Mwamashimba,ambapo pamoja na mambo mengine Mgeja katika hotuba yake alwataka wananchi kuendelea kuiamini ccm kwani ndiyo mwarobaini wa matatizo yao hivyo wawapuuze wapinzani wanaoendekeza matusi na sasa wanadiriki hadi kutukana waasisi wa taifa hili akiwemo baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere na matokeo yake pia kuanza kupuuza muungano wa Tanganyika na Zanzibar |
|
Ni katika eneo la mkutano wa kwanza kushoto ni MNEC,Boniface Butondo,katikati ni katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago,akifuatiwa na mwenyekiti wa wazazi ccm mkoa wa Shinyanga ndugu Wile Mzava wakifurahia jambo katika eneo la mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwamashimba wilayani Kishapu wakati wa ziara ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuangalia namna ilani ya ccm inavyotekelezwa |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com