Mkutano unaendelea,wananchi na viongozi wa chama wakifurahia burudani katika eneo la mkutano |
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kishapu Shija Malisha Nteleju akimkaribisha mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ili azungumze na wananchi wa kijiji cha Mwamashimba,ambapo pamoja na mambo mengine Mgeja katika hotuba yake alwataka wananchi kuendelea kuiamini ccm kwani ndiyo mwarobaini wa matatizo yao hivyo wawapuuze wapinzani wanaoendekeza matusi na sasa wanadiriki hadi kutukana waasisi wa taifa hili akiwemo baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere na matokeo yake pia kuanza kupuuza muungano wa Tanganyika na Zanzibar |
Ni katika eneo la mkutano wa kwanza kushoto ni MNEC,Boniface Butondo,katikati ni katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago,akifuatiwa na mwenyekiti wa wazazi ccm mkoa wa Shinyanga ndugu Wile Mzava wakifurahia jambo katika eneo la mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwamashimba wilayani Kishapu wakati wa ziara ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuangalia namna ilani ya ccm inavyotekelezwa |
Social Plugin