Askofu Simon Masunga wa kanisa la Tanzania Assemblies of God
lililopo Geita Mjini mara baada ya kumaliza mahubiri katika viwanja vya
Kalangalala mjini Geita
|
Wananchi
mkoani Geita wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vikongwe kwa imani za
kishirikina na wale wanaoua wahalifu wametakiwa kuacha tabia hiyo
mara moja kwani wanaenda kinyume na maandiko matakatifu ya yesu kiristo.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Asikofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assembies of God
(T.A.G).jimbo la Geita Simon Masunga kwenye mkutano wa siku 8 unaoendelea katika
viwanja vya Kalangalala vilivyoko mjini Geita.
Lengo la mkutano huo ni kuwahubiri wakiristo wa
mkoa wa Geita wanaowaua vikongwe na kuwachoma moto wahalifu ili waachane na
vitendo hivyo na kumrudia mwenyezi mungu.
Askofu
Masunga watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vikongwe
kwa pamoja na kuwachoma moto wahalifu hawamjui mwenyezi mungu na
wamejikita kwenye mambo mengi ya kidunia kuliko kumweka mungu mbele.
Ameongeza
kuwa yeye kama askofu na waumini
wanajitahidi kuwaombea waumini ili waokolewe na kuacha dhambi hiyo.
Katika
hatua nyingine askofu Masunga amewakemea wachungaji wanaofungua makanisa kwa
ajili ya uchochezi au kukashifu dini nyingine kuacha tabia hizo na badala yake
wafanye kazi ya mungu ili watu waokoke na kutenda yaliyo mema mbele za mungu.
Askofu
huyo ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kulegeza masharti
ya vibali vya kufanya mikutano kwani masharti ni magumu na mizunguko inakuwa mingi sana mpaka kupata
vibali vya mikutano.
Na
Valence Robert- Geita.