Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Geita Leo-ASKOFU MASUNGA ALIA NA WANAOUA VIKONGWE,AKEMEA WACHUNGAJI WANAOFUNGUA MAKANISA KWA AJILI YA UCHOCHEZI

Askofu Simon Masunga wa kanisa la Tanzania Assemblies of God lililopo Geita Mjini mara baada ya kumaliza mahubiri katika viwanja vya Kalangalala mjini Geita
Wananchi mkoani Geita wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vikongwe kwa imani za kishirikina na wale wanaoua wahalifu wametakiwa  kuacha tabia hiyo mara moja kwani wanaenda kinyume na maandiko matakatifu ya yesu kiristo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Asikofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assembies of God (T.A.G).jimbo la Geita Simon Masunga kwenye mkutano wa siku 8 unaoendelea  katika viwanja vya Kalangalala vilivyoko mjini Geita.

 Lengo la mkutano huo ni kuwahubiri wakiristo wa mkoa wa Geita wanaowaua vikongwe na kuwachoma moto wahalifu ili waachane na vitendo hivyo na kumrudia mwenyezi mungu.

Askofu Masunga   watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vikongwe kwa pamoja na kuwachoma moto wahalifu hawamjui mwenyezi mungu na wamejikita kwenye mambo mengi ya kidunia kuliko kumweka mungu mbele.

Ameongeza kuwa  yeye kama askofu na waumini wanajitahidi kuwaombea waumini ili waokolewe na kuacha dhambi hiyo.

Katika hatua nyingine askofu Masunga amewakemea wachungaji wanaofungua makanisa kwa ajili ya uchochezi au kukashifu dini nyingine kuacha tabia hizo na badala yake wafanye kazi ya mungu ili watu waokoke na kutenda yaliyo mema mbele za mungu.

Askofu huyo ametumia fursa hiyo kuiomba serikali  kulegeza  masharti ya vibali vya kufanya mikutano kwani masharti ni magumu  na mizunguko inakuwa mingi sana mpaka kupata vibali vya mikutano.


Na Valence Robert- Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com