Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hatari Kweli Kweli!!! KIBOKO AUA MTU HUKO SIMIYU,ILIKUWA VITA KALI KATI YA KIBOKO NA WANANCHI


Kijana  mmoja  mkazi wa kijiji cha Malili kata ya Malili Wilayani Busenda mkoani Simiyu Japhet Nhandi(18) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya na mnyama aina ya kiboko.

Tukio hilo limetokea jana wilayani humo baada ya wananchi kupambana na mnyama huyo,kitu kilichopelekea kumuua kijana huyo.

Kaka wa marehemu aliyekuwepo katika tukio hilo John Nhandi, ameiambia Radio Kahama FM kuwa tukio hilo limetokea saa 10 jioni kijijini humo wakati wa mapambano na mnyama huyo.

Amesema baada ya kujeruhiwa vibaya walifanya utaratibu wa kumpeleka mdogo wake katika hospitali ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza,lakini wakati wakiwa njiani alifariki dunia kutokana na kujeruhiwa sana na mnyama huyo. 

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Busenda Kitusi Kamani (CCM),ambaye amehudhuria mazishi hayo kama sehemu ya mshikamano na kuwapa pole wafiwa, amesema wanachi wilayani humo wanatakiwa kuwa makini na wanyama pori wanaoingia kijijini humo.

Mbunge Kamani yupo wilayani Busenda kwa mapumziko na kuendelea kuhamasisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika jimbo lake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com