Kulia ni mwili wa marehemu baada ya kuchomwa moto-kushoto ni Machela ikiandaliwa kuupakia mwili wa kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto |
Kijana aliyejulikana kwa jina la Mangi akiwa ndani ya gari, pembeni yake ni maiti ya mwenzake |
Polisi wakikagua makoti ambayo kijana aliyenusurika alikuwa ameyavaa |
Mtu mmoja anaesadikiwa
kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina anayekadiliwa kuwa na umri wa
miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na mwingine
kunusurika kuuwawa.
Tukio
hilo limetokea jana
alfajiri katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani
Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia
jana katika mtaa wa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya
solar
ziliibiwa.
Katibu wa Sungusungu
katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa kufuatia tukio hilo
waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji vyote na ndipo
walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana mwingine
aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai wanatafuta
pikipiki iliyopotea.
Mashalia ameongeza kuwa
kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara ikiwa ni
pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.
Kwa upande wake mkaguzi
msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka wananchi wa kata
hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba wawasiliane na uongozi
wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.
Social Plugin