Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Heeeh!! WAFUTIWA KESI YA UBAKAJI BAADA YA KUKUBALI KUMUOA MSICHANA WALIYEMBAKA

Kwa mujibu wa Daily Mail, mafisa hao waliotajwa kwa majina ya Sachin Gupta (27) na Saurab Chopra (25) walikuwa wakishitakiwa kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 21 ndani ya hotel huku wakichukua video ya tukio hilo kwa kutumia simu zao za mkononi.
Familia za maafisa hao zilitoa pesa nyingi kwa familia ya msichana aliyebakwa ili wawasamehe watu hao na kuachana na kesi hiyo.
Ingawa familia hiyo ilizipokea pesa hizo, bado waliwapa masharti kuwa watuhumiwa wamuoe binti walimbaka na mdogo wake mwenye umri wa miaka 19 ndipo ombi lao litakapokubaliwa.
Baada ya pande zote mbili kukubaliana, ndoa ilifungwa katika eneo la Bareilly, jijini Uttar Pradesh. Hata hivyo, mabwana harusi hao waliokuwa bado wako jela hawakuhudhuria tukio hilo kwa kuwa hawakuruhusiwa hadi pale ndoa ilipofungwa rasmi.
Baada ya taratibu za ndoa kukamilika na wao kutangazwa rasmi kuwa wanandoa, ndipo walipoachiwa huru kutoka jela.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com