Helikopta waliyokua wakisafiria Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal,
waziri wa ujenzi John Magufuli, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es
salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick
imepata ajali asubuhi wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege Dar es
salaam. (kwa mujibu wa mashuhuda)
Taarifa zilizotoka muda mfupi baadae zimeeleza kupata majeruhi lakini
hakuna yeyote aliepoteza maisha baada ya Helikopta hiyo kuanguka wakati
ikianza safari kuwapeleka viongozi hao kutembelea maeneo yaliyoathirika
na mafuriko.
Wote walitoka salama na majeraha madogomadogo ambapo pia kwenye
taarifa nyingine iliyotolewa na TBC, wameendelea na ziara ya kutazama
athari za maafuriko kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo Pwani.
Ajali hii ya Helikopta imetokea siku moja baada ya ndege ya shirika
la ndege la Kenya kubamiza chini na kuharibu upande wa kulia wa bawa
kutokana na ukungu mkubwa uliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Dar es
salaam wakati ikitua kutokea Nairobi, hakuna aliepoteza maisha ila
waliojeruhiwa wakati wa kushuka kwa dharura kutoka kwenye ndege.
Taarifa
kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema
wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa
ndege Dar es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia
paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha
aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote
alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji
helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua
inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam
ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka.
Picha zote mbili kutoka nasmamafoto.blogspot.com
Social Plugin