Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo |
Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti
Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu mbalimbali .
Uharibifu mkubwa na wahatari ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.
Katika eneo la Mlalakuwa mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika kabisa na nyingine mbili zimelegea katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni mti huo si mkavu ni mbichi.
Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?
Tunaomba muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae kwani ni hatari sana
via>>Dar es salaam yetu Blog