Licha Ya Jeshi la Polisi Kuendelea Kukabiliana na Matukio Ya Mauji Ya Kulipizana Visasi na Imani za Kishirikina Lakini Matukio Ya Mauaji Ya Kutisha Yanaendelea Kushamili Mkoani Njombe Siku Hadi Siku Hali Inayohatarisha Ustawi wa Maisha Ya Wakazi wa Mkoa wa Njombe
Machi 30 Mwaka Huu Huko Katika Kijiji cha Lole Kata ya Ikuna Wilayani Njombe Yametokea Mauaji Ya Kutisha Baada Ya Mwalimu wa Shule Ya Msingi Lole Kuuawa Kikatili.
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kwamba Majira Ya Saa 4:30 Usiku Katika Kijiji Hicho Cha Lole Mwalimu wa Shule Ya Msingi Lole Luchabiko Ngimbudze Mwenye Umri wa Miaka 55 Aliuawa na Mtu/Watu Wasiofahamika Kwa Kupigwa na Kitu Kizito Usoni.
Taarifa Ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Imeeleza Kuwa Baada ya Mwalimu Huyo Kupigwa na Kitu Kizito Usoni Pia Alifungwa na Shati Shingoni.
Taarifa Hiyo Imefafanua Kuwa Marehemu Aliuawa Baada ya Wauaji Hao Kuvunja Mlango wa Nyumba Yake na Kuingia Ndani Hadi Chumbani Kwake.
Katika Hatua Nyingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Amesema Kitendo cha Wananchi Kuendelea Kujichukulia Sheria Mkononi Hakifai Katika Jamii na Hivyo Kinapaswa Kupigwa Vita Kwa Kila Mmoja Wetu.
Hata Hivyo Jeshi Hilo Limetoa Wito Kwa Mtu Au Watu Wenye Taarifa Ya Watu Waliohusika na Tukio Hilo Ili Hatua Za Kisheria Ziweze Kuchukuliwa Dhidi Yao.
Na Gabriel Kilamlya- Njombe