Mahakama kuu
inayoendelea mjini Geita mkoani Geita imemhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa Mathias
Tangawizi(46) mkazi wa kijiji cha Ibondo katika kata ya Katoro wilayani Geita baada ya kupatikana na kosa la kumuua mama mkwe wake aitwaye Sofia
Kamuli (51)mwaka 2008.
Akisoma
hukumu hiyo jaji wa mahakama kuu Richard Malima amesema kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa hilo tarehe 24 mei 2008 ambapo inadaiwa kuwa mama mkwe
alikuwa anamtaka mtoto wake aachane na mme wake kwani alikuwa na uwezo mdogo wa
kimaisha na baada ya kupata taarifa hizo mtuhumiwa ndipo alipotenda kosa hilo
dhidi ya mama mkwe wake.
Awali
mwanasheria wa serikali Emiri Kiria aliiambia
mahakama kuwa mnamo tarehe 24 mei 2008 huko katika kijiji jirani cha Kaduda katika kata ya katoro majira
ya saa 3.30 asubuhi mtuhumiwa alimfuata mama huyo na kumchoma mkuki sehemu za
shingoni na tumboni hadi kufa.
Baada ya kufanya mauaji hayo kwa kuchoma mkuki mama mkwe wake Sofia
Kamuli (51)ambaye alikuwa mkulima,Mathias Tangawizi alimtoa nje
marehemu kwa kumvutia ndani na kufunga milango huku akitokomea
kusikojulikana.
Ameongeza
kuwa baada ya siku mbili mtuhumiwa huyo alikamatwa kwani alikuwa amerudi
katika kijij chake cha Ibondo ndipo jeshi la polisi lilimtia hatiani kwa kuhusika
na mauaji hayo.
Aidha
ushahidi uliotolewa na mashahidi saba kwa mfululizo umekuwa wa kuridhisha dhidi
ya mtuhumiwa ambao haukuwa na mashaka yoyote hivyo na kuiomba mahakama itoe
adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutaka
kutenda unyama huo.
Mara baada
ya mahakama kusikiliza pande zote za mtuhumiwa na mlalamikaji ilijiridhisha
kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa kudhamiria hivyo mahakama ikaamua kumtia
hatiani kwa kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa kifungu cha 197 sura ya 16 cha
mwaka 2002.
Kwa upande
wa mtuhumiwa alijitetea kuwa apunguziwe adhabu kwa amekaa mahabusu kwa uUda
mrefu hivyo angeweza kupunguziwa adhabu vilevile alijitetea kuwa mara baada ya
kuingia mahabusu amekuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali hivyo apunguziwe
adhabu lakini Mahakama ilitupilia mbali maombi ya mtuhumiwa huyo.
Na Valence Robert- Geita
Social Plugin