KIFO CHA MCHEZA DENSI CHASABABISHA VURUGU KATI YA POLISI NA WANANCHI

_74389174_d0b6bc11-91fd-4ff7-acfc-b482ee3227ed
Kutoka Brazil Kumezuka mapigano kati ya jeshi la polisi na
wakazi wenye hasira usiku kucha katika moja ya viunga vya mji mkuu Rio de Janeiro ambapo Barabara zilifungwa mjini humo wakati risasi zikisikika kutoka eneo hilo na polisi waking’ang’ana kuwadhibiti wakaazi hao.

Ghasia hizo zilianza baada ya kifo cha mwanamume mwenye umri wa miaka 26 aitwaye Douglas Rafael da Silva ambaye ni mchezaji densi wa kulipwa ambapo familia yake iliupata mwili wake  ukiwa umejaa vidonda na kuwalaumu maafisa wa polisi kwa kumpiga hadi kufa baada ya kumhisi kuwa mwanachama wa genge moja linalouza madawa ya kulevya.
Watu walikusanyika katika lango la kuingia katika makazi hayo ya mabanda sehemu alikopatikana mtu huyo akiwa ameauwa na wakataka kujua kutoka kwa maafisa wa polisi sababu za kuuliwa kwake,Polisi kadhaa wa kijeshi wenye silaha wako mahali hapo kufuatia habari kuwa kituo cha polisi kilichoko mahali hapo kimevamiwa.
_74385484_022003268-2
Pavaozinho ni miongoni mwa makaazi ya mabanda ambayo Serikali Kuu ya Brazil imejaribu kuwatimua magenge ya wauzaji wa madawa ya kulevya wenye silaha kutoka kwa jamii na kueneza amani na mamlaka ya polisi.

Polisi wamekiri katika mahojiano na BBC kuwa wameshindwa kudhibiti usalama katika makaazi ya mabanda katika mji mkuu wa Rio de Jenairo,muda mfupi tu wakati ambapo wageni wengi wanatarajiwa kuingia nchini humo ambao maelfu ya watu wanatarajiwa kuwepo nchini Brazil kwa sababu ya Kombe la Dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post