Kijana Mmoja aliyetuhumiwa kuwa Kibaka Akiwa amesimama kwa Huruma mara baada ya Kushushiwa Kipigo na wanaodhaniwa kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe cha Mjini Morogoro.
Wanafunzi wa Chuo Kukuu Mzumbe wamemkamata Kijana Mmoja anayesadikiwa kuwa kibaka kwenye moja ya Mabweni yao akijaribu kuiba vitu mbali mbali na kisha kumshushia kichapo hadi kupoteza maisha.
Tukio hilo lilitokea saa nane usiku ambapo kibaka huyo anayeisha nje ya Chuo hicho alikamatwa na mmoja wa wanafunzi ndani ya Bweni akiwa na lundo la Nguo na viatu.
Shuhuda wa tukio hilo alisema wwa muda mrefu wanafunzi hao walilalamika kuibiwa vitu vyao na watu wasiowafahamu.
Kibaka huyo aligoma kutua mizigo hiyo jambo linalodaiwa kuzidisha hasira kwa Wanafunzi hao na kuzidisha kumshambulia.
Kibaka huyo aligoma kutua mizigo hiyo jambo linalodaiwa kuzidisha hasira kwa Wanafunzi hao na kuzidisha kumshambulia.
Baada ya kukithiri kwa vitendo hivyo Chuoni hapo Wanafunzi waliamua kuongeza umakini wa kubaini mwizi wao ambapo mmoja wa wanafunzi ambaye alikuwa akijisome alisikia kishindo cha mtu kwenye Korido la Bweni lake ambapo baada ya kuchungulia alimshuhudia kibaka huyo akitoka na vitu mbali mbali ndipo alipoamua kupiga mayowe ya Mwizi yaliowaamusha wenzake ambao walimzingira kibaka huyo na kumkamata akiwa na kithibiti mkonono
"Madent hao waliokuwa na hasira walidaiwa walimpiga mwizi huyo ambaye kwa mashangao wa wengi kilicha ya kichapo hicho aligoma kuachia mazigo hiyo jambo lililozidisha hasira kwa madent hao na kuamu kuongeza kasi ya kumpiga na kudaiwa kumuua",
alisema Shuhuda huyo
Social Plugin