|
Ni katika
eneo la shule ya Msingi Kolandoto kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga
ambako leo kumefanyika kikao cha makamanda
wa jeshi la jadi sungusungu maarufu kwa jina la SANJO kutoka katika wilaya ya
Shinyanga vijijini,Shinyanga mjini na wilaya ya Kishapu lengo likiwa ni
kujadili namna ya kukabiliana na tatizo la uharibifu wa miundombinu kama vile
ya umeme,maji,barabara,reli na kampuni ya simu ya TTCL pamoja na tatizo la
wanafunzi kutoripoti shuleni wanapochaguliwa kuingia kidato cha kwanza.Mgeni
rasmi alikuwa ni Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi aliyekuwa
mgeni rasmi katika kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Annarose Nyamubi
|
|
Katibu
tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao
hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akitafkari
jambo katika kikao hicho kilicholenga kujadili namna ya kukabiliana na tatizo
la uharibifu wa miundombinu kama vile ya umeme,maji,barabara,reli na kampuni ya
simu ya TTCL pamoja na tatizo la wanafunzi kutoripoti shuleni wanapochaguliwa
kuingia kidato cha kwanza.Katikati ni mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga
Richard Ngede akifuatiwa na mkuu wa usalama wilaya ya Shinyanga Hosea
Chikorongo.Mwenye kofia ni mwenyekiti wa sungusungu wilaya ya Shinyanga mjini bwana Jiganza Jidula
|
|
Diwani wa
kata ya Kolanadoto kulikofanyika kikao hicho cha makamanda wa jeshi la jadi
sungu sungu,bi Agnes Machiya akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema
kikao hicho kitakuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika jamii katika
kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya umeme,maji
n.k,uharibifu amabo umekuwa ukifanywa na wanajamii wenyewe.
|
|
Mwenyekiti wa sungusungu wilaya ya Shinyanga mjini bwana Jiganza Jidula akifungua kikao hicho maarufu kama SANJO kilichokutanisha makamanda wa sungusungu kutoka wilaya tatu katika mkoa wa Shinyanga,ambapo sungusungu wameitisha kikao hicho ili kuangalia namna ya kukabiliana na wahalifu wanaoharibu miundombinu hiyo kama vile kuiba nyaya za umeme,kuiba mafuta ya transfoma,kung'oa mataluma ya reli,kuharibu madaraja n.k |
|
Katibu
tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao
hicho ambapo akizungumza katika kikao hicho kilichokutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile viongozi wa TANESCO,SHUWASA,KASHWASA,TANROADS,TTCL ,waandishi wa habari ambapo alisema ni vyema suala la ulinzi wa miundombinu likafanywa na kila mtu huku akiwataka wananchi kuwafichua wanaofanya uharibifu kwani wananchi wanajua kwa vile wanaishi nao katika jamii matokeo yake kuleta athari kiuchumi na kijamii pale miundombinu inapoharibiwa
|
Afisa
uhusiano na wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga bwana Amoni Michael akizungumza wakati
wa kikao cha makamanda wa jeshi la jadi sungusungu maarufu kwa jina la SANJO
kutoka katika wilaya ya Shinyanga vijijini,Shinyanga mjini na wilaya ya Kishapu
.
Aliwataka
Sungusungu kusaidiana na shirika hilo pamoja wananchi kuwabaini wanaohujumu
miundo mbinu kama vile mita,transimita,nguzo na nyaya kuna athari kubwa
kiuchumi na kijamii na kwamba shirika hilo litatoa zawadi kwa yeyote atakayetoa
taarifa sahihi kuhusu wanaohujumu miundombinu pia aliwataka wananchi kutofanya
shughuli yoyote ya kiuchumi kama vile kulima katika eneo la njia ya Umeme na
kwamba na wahesabu mita 30 kulia na kushoto kuanzia kwenye njia ya umeme.
|
. |
|
Mhandisi wa njia kuu za umeme(TANESCO)mkoa wa Shinyanga Job Bidya akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema hujuma za miundombinu zinapofanyika serikali inapata hasara kubwa lakini pia athari za kiuchumi na kijamii zinatokea mfano kama huduma ya umeme haipo inaathiri hata upatikanaji wa maji na ghrama za bidhaa kupanda |
|
Mkuu wa kituo polisi reli mkoa wa Mwanza Suzana Kidiku akizungumza katika kikao hicho ambapo pamoja na mambo mengine alisema miundombinu ya reli imekuwa ikiharibiwa kutokana na wananchi kuiba vyuma vya reli na kuvigeuza kuwa vyuma chakavu na wengine kutumia kutengeza majembe ya pilau,lakini hivi sasa wamebaini kuwa watoto wanaochunga mifugo wamekuwa wakiiba mataluma na wengine kuweka mawe relini hivyo kuwataka viongozi wa sungusungu kuwapa ushirikiano katika kupiga vita uharibifu wa miundombinu na kwani miundombinu inapoharibiwa zinaweza kutokea ajali,gharama za bidhaa kupanda. |
Mwakilishi wa meneja wa TANROADS mkoa wa Shinyanga bwana Julius Rweyemamu akizungumza katika sanjo hiyo ambapoa aliwataka wanachi kuacha kujenga kwenye hifadhi za barabara pamoja na kuacha tabia ya kuweka matuta katika barabara na kuwaasa wananchi wote kuwa walinzi wa miundombinu
|
Mkuu wa
polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede akizungumza leo katika kikao cha
viongozi wa Jeshi la jadi sungusungu wilaya za Kishapu,Shinyanga mjini na
Shinyanga mjini ambapoa alilitaka jeshi la sungusungu pamoja na wananchi kwa ujumla
kuzingatia utii wa sheria bila shuruti wanapokamata wahalifu kwa kutumia nguvu
ya kadri badala ya kutumia nguvu kubwa kuwaadhibu wahalifu.Pia aliwataka
viongozi wa sungusungu na wananchi wanapokamata wahalifu kutokaa nao muda mrefu
bali wawafikishe kwenye vyombo vya sheria huku akiwataka jeshi la sungusungu
kufanya marekebisho katika sheria na taratibu zao kama vile kuwatenga wananchi
katika huduma za jamii.
|
|
Mmoja kati ya makamanda wa sungusungu akichangia mawili matatu katika kikao hicho ambapo alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa wanapokutana ama kukamata wahalifu mfano kuna baadhi ya wahalifu wanakuwa na silaha za moto,lakini pia hawana usafiri
|
|
Meneja wa kampuni ya simu ya TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kaguru akizungumza katika sanjo hiyo ambapo alisema kuharibiwa kwa miundombinu kunafanywa na wananchi wasio waaminifu hivyo kuitaka jamii kutowafumbia macho na TTCL pia inatoa zawadi kwa mtu yeyote anatoa taarifa sahihi na yenye vielelezo juu ya wanaohujumu miundombinu yao kama vile kuiba cable walizozitandaza chini ya ardhi(Mkongo wa taifa)
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553